Kutokana na kikithiri kwa mmomonyoko wa maadili nchini, vijana Mkoani Lindi wamehimizwa kuepuka kufuata mkumbo na kutafuta furaha kwa kufanya matendo yasiyofaa na badala yake watumie ujana wao katika mambo ya msingi ikiwemo ya kiimani na kijamii.



Na Elizabeth Msagula

Yamekumbushwa hayo Januari 28, 2023 na Askofu wa kanisa katoliki Jimbo la Lindi Mhashamu Wolfgan Pisa wakati wa adhimisho la misa takatifu ya Vijana wa Katokili walio katika vyuo na shule za Sekondari katika Mikoa ya Lindi na Mtwara iliyofanyika katika kanisa la Mtakatifu Andrea Kagwa, ibada iliyohudhuriwa pia na katibu Tawala wa Mkoa wa Lindi Ngusa Samike.

Kwa upande wake Katibu Tawala wa Mkoa wa Lindi Ngusa Samike  amewakumbusha vijana hao kufanya matendo ya huruma katika jamii ikiwemo kutoa misaada kwa watu mbalimbali na kuhakikisha wanakuwa faraja kwa wazazi wao badala ya kuwachukiza na kuwaumiza kwa matendo yasiyofaa kama kujiingiza kwenye matumizi ya madawa ya kulevya na mahusiano ya jinsia moja.

Pia amewakumbusha umuhimu wa kumtumikia Mungu pamoja na kuwataka kuendelea kudumisha mshikamano ili kuwa na Taifa imara.

Nao baadhi ya vijana akiwemo Jonas Stenslaus na Annastansia Kahama kutoka chuo cha 'Lindi Health and Science' wameomba viongozi wa dini na wazazi kuendelea kuwalea katika maadili mema ili kuepukana na changamoto ambazo wanakutana nazo na kukua katika misingi mizuri ya kidini.

Post a Comment

Previous Post Next Post