Rai  imetolewa kwa Asasi za Kiraia  zinazotekeleza Miradi ya afya katika Mkoa wa Mwanza na Shinyanga kuendelea kuwa na desturi ya kufanya kazi kwa kushirikiana na Halmashauri ili  kushirikisha jamii   katika uimarishaji wa huduma bora za afya na kuleta mabadiliko chanya.


Baadhi ya wawakilishi wa asasi mbalimbali za kiraia kutoka baadhi ya halmashauri ya mikoa miwili ya Mwanza na Shinyanga wakifuatilia mafunzo ya Tathmini Shirikishi ya Kijamii (Community Score Card) ambayo ni moja ya Afua ya Ushirikishaji Jamii  yanayoratibiwa na Wizara ya Afya, Idara ya Kinga, Elimu ya Afya kwa Umma, Mpango wa Huduma za Afya ya Jamii kwa kushirikiana na AMERICARES Kupitia Mradi wa UZAZI STAHA

Rai hiyo imetolewa leo Januari 30,2023 Wilayani Sengerema mkoani Mwanza  na Mratibu wa Huduma za Afya katika jamii kutoka Ofisi ya Rais ,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa [OR-TAMISEMI] Martha Mariki katika ufunguzi wa mafunzo ya Tathmini Shirikishi ya Kijamii (Community Score Card) ambayo ni moja ya Afua ya Ushirikishaji Jamii  yanayoratibiwa na Wizara ya Afya ,Idara ya Kinga, Elimu ya Afya kwa Umma, Mpango wa Huduma za Afya ya Jamii kwa kushirikiana na AMERICARES Kupitia Mradi wa UZAZI STAHA.

Martha amesema ni muhimu, Asasi za Kiraia kushirikiana  na Serikali  katika kuwezesha Maendeleo hususan  Sekta ya Afya.

“Moja ya kitu ambacho tunakiamini ni Community Empowerment ,Usipoweza kufanya community Empowerment wananchi watakuwa tegemezi badala ya wao kushiriki kufanya mambo fulani ya kuleta maendeleo na  watakuwa wanaisubiri serikali kupeleka huduma,hivyo sisi kama Asasi za Kiraia na Serikali kwa ujumla ni muhimu kushirikisha jamii na itatupeleka pazuri  kwa maendeleo ya Sekta ya Afya”amesema.

Dkt.Rebecca Mdee Mkufunzi mwezeshaji wa Mafunzo ya Tathmini shirikishi ya Kijamii akitoa mafunzo  ya Afya  shirikishi  ngazi ya jamii kwa  wawakilishi kutoka asasi za Kiraia mikoa ya Mwanza na Shinyanga yanayofanyika Wilayani Sengerema Mkoani Mwanza.

Aidha,Martha  amesema ni muhimu kufanya kazi kama timu baina ya serikali na asasi mbalimbali za kiraia ili kuleta ufanisi katika sekta ya Afya.

“Katika Sekta ya Afya ukifanya kivyako bila kushirikiana na wengine ni rahisi sana kufeli,lakini ukifanya kama  timu tunajijengea imani kuwa tunaweza kuifanya kazi yetu kwa uhakika na bila kuchosha akili,nia madhubuti  ya kushirikisha kundi hili la asasi za kiraia [CSO,s] nia yetu ni kutusaidia kupeleka mafunzo katika halmashauri namna zinavyotoa mafunzo kwenye jamii” amesema.

Baadhi ya wawakilishi wa asasi mbalimbali za kiraia kutoka baadhi ya halmashauri ya mikoa miwili ya Mwanza na Shinyanga wakifuatilia mafunzo yaTathmini Shirikishi ya Kijamii (Community Score Card) ambayo ni moja ya Afua ya Ushirikishaji Jamii  yanayoratibiwa na Wizara ya Afya, Idara ya Kinga,Elimu ya Afya kwa Umma, Mpango wa Huduma za Afya ya Jamii kwa kushirikiana na AMERICARES Kupitia Mradi wa UZAZI STAHA

Kwa upande wake Mwakilishi kutoka Wizara ya Afya, Idara ya Kinga Sehemu ya Elimu ya Afya kwa Umma Orsolina Tolage amesema, serikali itaendelea kuandaa Miongozo ya utekelezaji wa shughuli mbalimbali za Huduma za Afya ikiwemo afua hii ya Tathmini Shirikishi ya Kijamii ambapo mafunzo hayo yatasaidia kuwajengea uwezo wawakilishi kutoka Asasi za Kiraia kuwa na mipango ya pamoja itakayosaidia kuleta mabadiliko chanya na kuendelea  kuboresha huduma za afya.

Mafunzo haya yatawajengea uwezo namna gani wataweza kutekeleza hatua za ushirikishaji jamii katika kutekeleza afua ya ushirikishwaji wa jamii kutatua changamoto na kuweka mipango madhubuti ya kuweza kutekeleza pale ambapo wanaona hapafanywi vizuri, mfano, kwenye vituo ambapo wanapata huduma wananchi na tathmini shirikishi hii ya kijamii inashirikisha wananchi kukaa kwa pamoja kujadili na kuweza kuweka mpango mkakati wa namna ya kuiondoa ile changamoto ili waweze kuboresha huduma kwenye vituo vyao” amesema.

Ikumbukwe kuwa Mafunzo hayo ya tathmini shirikishi ya jamii sekta ya afya  yanatolewa kwa asasi za kiraia kutoka mikoa ya Mwanza kwa halmashauri ya Magu, Sengerema, Ukerewe na Misungwi na Mkoa wa Shinyanga kwa Halmashauri  ya Msalala, Kishapu na Manispaa ya Shinyanga.

Post a Comment

Previous Post Next Post