YOUR FUTURE IS CREATED BY WHAT YOU DO TODAY, NEVER TOMORROW

Serikali ya nchi ya Zimbabwe imeingia katika majadiliano makubwa baada ya tatizo la umeme kuwa kikwazo katika shughuli za kimaendeleo ikiwemo viwanda. hii imekuja baada ya kuonekana kwamba ushuru unaotozwa kwa sasa na huduma zinazopatikana hususani zile zinazohusisha umeme kutowaridhisha wananchi na watendaji pia.

Tatizo hili nchini Zimbabwe limekuja baada ya Bwawa kubwa na maarufu kwa uzalishaji wa umeme, KARIBA kupungua maji yake ndani ya mwaka huu. Bwawa hilo kwasasa liomekuwa likizalisha Megawati (MW) 358 kutoka katika kiwango chake cha kawaida ambapo huzalisha Megawati (MW) 542 kwa siku.

Bwawa la Kariba

Hali hii imefanya wananchi na wazalishaji wa bidhaa na huduma tofauti viwandani kukosa umeme zaidi ya masaa 16 kwa siku. George Guvamatanga ambaye ni katibu mkuu katika Wizara ya Fedha na Uchumi nchini humo, ameeleza kuwa suala la umeme liko katika nafasi za juu katika mikakati na mijadala ya serikali. 

Pia ameeleza kuwa wanatambua kuwa ushuru wa kodi za umeme uko juu na hata serikali haiwezi kumudu kwa urahisi tatizo hilo ambalo litatatuliwa hivi karibuni.

Post a Comment

Previous Post Next Post