YOUR FUTURE IS CREATED BY WHAT YOU DO TODAY, NEVER TOMORROW

Kabla ya mkataba wake kuvunjwa, Amunike alisema kutolewa mapema nchini Misri ilikuwa ni funzo kubwa kwa Tanzania.
"Ni somo kubwa kwa mpira wa Tanzania. Hatukuwahi kushiriki toka mwaka 1980, mambo mengi yametokea ndani ya miaka 39, na mpira umebadilika na unaendelea kubadilika,"
"Kitu cha msingi ni kuendana na mabadiliko haya na kuimarika kama timu. Kuna mengi ya kujifunza.
"Shida yetu kubwa ilikuwa ni kutokuwa na uzoefu. Hatuna uzoefu wa kutosha sababu tumezoea kucheza mpira bila kuwa na shinikizo kubwa."
"Lakini tumeona katika michuano hii pale unapokuwa na mpira, basi wapinzani wanakuweka katika shinikizo kubwa."
"Katika kila safari, kuna mchakato wa kujifunza. Tutakaporejea (nyumbani) itatupasa tujitathmini kwa undani na kuona ni kwa namna gani tutaboresha mpira wetu.
"Ni dhahiri kuwa katika mpira wa kisasa, kama huna uwezo wa kushindana hutakuwa na nafasi ya kushinda - na hilo ndilo tulilokutana nalo."
"Kama tutaendelea na ari hii, na kuboresha katika yale tufanyayo naamini tutakuwa kama timu."
Post a Comment