YOUR FUTURE IS CREATED BY WHAT YOU DO TODAY, NEVER TOMORROW
Kwa wale waongea KISWAHILI na kiingereza cha darasani, nani
kati yenu anataka nifanye ujinga ndipo mnisaidie?
Ni kiasi gani tunasisitizana kuwa na Upendo na kuwa na moyo
wa kusaidiana hata kugawana tulichonacho. Japokuwa si kila wakati nitakupa sawa
na nitakachobaki nacho mimi. Lakini si haya machache…!
Ajabu leo mtu anagawiwa maarifa eti kwa sababu anahisi kuna
manufaa kwa mgawaji tena hata asijue hakika yake, akapuuza alichostahili. Nani
ana nafasi mbili za mafanikio na ana hakika hata leo siyo masikini na aliyekosa
mafaniko aliyoyataka? Tusilishane ujinga na tukashangilia huku tukiendelea
kuwatazama macho meupe wanaotuzubaisha.
Nikiwa mtanzania ndani ya nchi yangu ambayo wakazi wake
walichagua lugha ya Kiswahili kutumika kama lugha ya taifa katika mawasiliano
na baadaye Kiingereza kama lugha ya ofisini, hii yote ni mali yangu. LUGHA.
Watoto tangu wanapokuwa wamefikia umri wa kuenda shule,
mwalimu wake wa elimu ya awali anamfundisha kutamka maneno mageni, na yale ya
lugha zinginezo yakiwemo. Kiingereza hata lugha za kibantu wakati wa
kueleweshana kati ya mwalimu na mwanafunzi haswa katika shule zipatikanazo
maeneo ya vijijini. Ahsante watanzania wote tunajua kusoma na kuandika na kama
huwezi vyote basi unaweza kutazama picha na ukaelewa.
Lakini,tusitumie uelewa wetu kama silaha za kuangamizana
wenyewe, maana ndivyo ilivyotakiwa kuwa toka katika dhamira ya aliyetuaminisha
hivyo. Bali tuone njia ya kuutafuta muafaka na kutatua haya machache ambayo
yanatokana na uchochezi wa haya mataifa MOTO MOTO, nayaita hivyo. Tumia uelewa
kujua lengo lao ni lipi na tunawezaje kutengeneza udhaifu katika ngwe hii
shuruti kwa vizazi vyetu tulivyonavyo na vijavyo hofu juu ya Vitakavokuwa vyao.
Lingekuwa jambo jepesi ningeandika mashairi kadhaa ukawa
mziki. Nimehitaji chombo cha habari, nacho kinanipatia changamoto tofauti. Iko
hivi …… Itaendelea
USIKOSE KUFUATILIA MACHAPISHO YA KILA SIKU ILI UPATE
KUFAHAMU NJIA MBALIMBALI ZA ULAGHAI MJINI HASA KATIKA TASNIA MAMA KWA VIJANA
WETU TANZANIA.
Tembelea kurasa zetu katika mitandao ya kijamii:
facebook | instagram
@muzikihuru
Post a Comment