Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imebaini uwepo wa baadhi ya vyombo vya moto vinavyotumia umeme (electrical vehicles) ambavyo havijasajiliwa wala kubandikwa vibao vyenye namba rasmi za usajili (Number plates) na hivyo inapenda kuutaarifu umma kuwa, kuanzia tarehe 16 Mei hadi 30 Juni 2025, watumiaji wote wa vyombo hivyo vikiwemo pikipiki, maguta na vinginevyo wanatakiwa kusajili na kubandika vibao hivyo ndani ya muda uliotolewa.

Takwa hili ni kwa mujibu wa Sheria ya Usalama Barabarani (The Road Traffic Act, 1973) Kifungu Namba 8 (1) kinachomtaka kila mtumiaji wa chombo cha moto barabarani kutimiza wajibu huo. Baada ya tarehe hiyo, hatua za kisheria zitachukuliwa kwa wale wote ambao hawatatekeleza jukumu hilo.

Aidha, TRA inaukumbusha umma kuwa, imefanya maboresho ya mfumo wa usajili wa vyombo vya moto kwa lengo la kurahisisha usajili wa vyombo vyote vinavyopaswa kusajiliwa kisheria. Mfumo huo unapatikana kupitia Tovuti ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (www.tra.go.tz) au Ofisi za TRA zilizopo nchi nzima.
Kwa msaada na taarifa zaidi, tafadhali wasiliana na TRA kupitia:

Tovuti: www.tra.go.tz
Namba za simu bila malipo: 0800 750 075 au 0800 780 078
WhatsApp: 0744 23 33 33

“Pamoja Tunajenga Taifa Letu”

Imetolewa na:
IDARA YA ELIMU KWA MLIPAKODI NA MAWASILIANO

Post a Comment

Previous Post Next Post