Serikali ya Tanzania kupitia wizara ya sayansi na teknolojia imesema, panya 100 waliopewa mafunzo ya kutegua mabomu na kubaini vimelea vya ugonjwa TB wamepata ajira nje ya nchi baada ya kufuzu.
Kulingana na taarifa hiyo, Panya (13) wamepelekwa Angola, (11) Azerbaijan, (58) Cambodia na (6) Ethiopia kwa ajili kutambua mabomu yaliyotegwa ardhini pamoja na utambuzi wa vimelea vya kifua kikuu.
Panya 12 wamepelekwa nchini Marekani kama panya wa maonesho (mabalozi) kwenye shamba la wanyama.
Kwa mujibu wa wizara hiyo, utekelezaji wa mradi huo umeendelea kuijengea sifa na kuitangaza Tanzania ambapo Panya anayeitwa Ronin alivuja rekodi ya dunia kwa kutambua mabomu 109 yaliyotegwa ardhini huko Cambodia. Panya mwingine Magawa naye alitambua mabomu 71.
DW
Post a Comment