Shirikisho la Soka Afrika (CAF) limesema kuwa Ripoti ya Mkaguzi imeonesha maboresho katika Uwanja wa Benjamin Mkapa hayawezi kukamilika kwa wakati kwa ajili ya kuandaa Mchezo wa Marudiano wa Fainali ya Kombe la Shirikisho uliopangwa kufanyika Mei 25, 2025
Taarifa ya CAF imeeleza kuwa (Kama ilivyotangaza awali) mchezo huo wa #Simba dhidi ya #RSBerkane unatarajiwa kuchezwa kwenye Uwanja wa Amaan, Zanzibar
Taarifa hiyo imeeleza kuwa CAF itaendelea kushirikiana na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Serikali ya Tanzania na Wadau wote kuhakikisha Uwanja wa Mkapa na viwanja vyote vinakuwa tayari kwa Mashindano ya Mataifa ya Afrika (CHAN) na kukidhi Kanuni na Viwango vya CAF yanayotarajiwa kuanza Agosti 2, 2025
Post a Comment