
Makamu Mwenyekiti wa ACT Wazalendo Tanzania Bara Isihaka Mchinjita Mei 15.2025 amekutana na viongozi wa Ngome ya Wazee kutoka kata 20 za Manispaa ya Lindi katika kikao kilicholenga kujadili mwelekeo wa chama kuelekea uchaguzi mkuu wa 2025
Katika mkutano huo, Makamu Mwenyekiti huyo aliwaeleza wazee hao kuwa chama chao kimeamua kushiriki kikamilifu katika uchaguzi kama sehemu ya utekelezaji wa 'Operesheni Linda Demokrasia' kampeni ya kulinda haki za kidemokrasia, usawa, na misingi ya utawala bora nchini
“Mwaka huu tunakwenda kupambana si kwa maneno bali kwa vitendo, hatutakubali CCM waendelee kuwadhulumu Watanzania kwa jina la uchaguzi, tunajipanga kusimama imara hadi haki itendeke, na tunahitaji nguvu yenu wazee kuhakikisha Taifa halidanganywi tena" -Mchinjita
Wazee walipokea kwa mikono miwili maamuzi ya chama chao kushiriki uchaguzi, wakisisitiza kuwa historia na uzoefu wao unaonesha wazi kuwa hakuna mafanikio yoyote yanayopatikana bila mapambano, walikumbushia juhudi walizozifanya katika uchaguzi wa mwaka 2010, wakisema walishiriki kwa karibu kulinda na kushinikiza matokeo sahihi yatangazwe, "hatutakuwa watazamaji, tumejifunza kuwa mafanikio yoyote hayaji yenyewe, lazima yapiganiwe"
Mkutano huo ni sehemu ya mwendelezo wa maandalizi ya ACT Wazalendo kuelekea uchaguzi, huku wazee wakiahidi kutoa mchango wao mkubwa katika kuhakikisha demokrasia inalindwa na sauti ya wananchi inasikika na kuheshimiwa.
Post a Comment