Katika maadhimisho ya siku 16 za Ukatili wa kijinsia ambapo kilele chake kinafikiwa leo Disemba 10, 2024, Mahakama ya Hakimu Mkazi Lindi imetafsiri Ukatili wa kijinsia kama 'kitendo anachofanyiwa mtu yeyote (mwanamke/mwanaume) kwa lengo la kudhuru au kuumiza kisaikolojia, kimwili, kiafya, kingono na kiuchumi.
Maeneo yanayoweza kutazamwa zaidi katika mapambano dhidi ya ukatili wa kijinsia mkoani Lindi, Illuminata Lutakana Hakimu Mahakama ya Mwanzo Manispaa ya Lindi anaeleza kuwa, Mahakama imejadili matukio ya ukatili katika makundi mawili; ngazi ya mahakama ya mwanzo ikitajwa kujeruhi, kushambulia na kudhuru ambapo haya yamedhihirika katika mashauri ya mirathi na migogoro katika ndoa.Kundi la pili ni ukatili wa kijinsia katika mashauri yaliyofikishwa Mahakama za juu ikiwemo ulawiti, ubakaji na rushwa ya ngono. Hivyo, kama jamii na wadau wataelekeza nguvu zaidi katika maeneo haya, udhibiti utakua kwa kiwango bora zaidi na kuunda jamii yenye ustawi.
Hata hivyo tafiti nyingi bado zimeonesha kwamba, wanawake ndio wahanga wakubwa wa ukatili wa kijinsia. Chukua hatua na kuwa sehemu ya furaha na tabasamu ya Tanzania isiyo na ukatili wa kijinsia.
Post a Comment