Mashujaa FM imezungumza na TAKUKURU kupitia kipindi cha Kuchele ili kujua hatua zilizochukuliwa na mamlaka hiyo kufuatia taarifa ya ACT Wazalendo na Justine Maengo ambaye ni Afisa Mwandamizi idara ya elimu kwa Umma amesema hawana taarifa rasmi kutoka chama hicho ambazo zinathibitisha kutokea kwa matukio ya Rushwa wakati huu wa mchakato wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa ukiendelea.
ACT Wazalendo kupitia kwa Katibu wa Chama hicho Ndugu Ahmad Machupa jana Novemba 07, 2024 katika mahojiano na mwanahabari wetu wameeleza kuwa, wagombea 6 wamejiondoa katika mchuano hali inayohusishwa na matukio ya rushwa huku mgombea 1 hajarudisha form baada ya kutishiwa uhai.
Pamoja na hayo, Maengo amesema wataichukua taarifa ya Chama cha ACT Wazalendo kama mtaji katika kufuatilia mwenendo wa matukio ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa ili kuzuia na kupambana na Rushwa.
Post a Comment