Chama cha ACT Wazalendo kupitia taarifa yake kwa umma iliyotolewa jana 07 Novemba, 2024 kupitia ukurasa wake wa Instagram wameeleza kuwa "Kuna mpango wa wasimamizi wa uchaguzi kuzichafua au kuziongezea taarifa fomu za kugombea ili kuwapotezea sifa za kuteuliwa wagombea wa chama hicho na vyama vingine vya upinzani nchini katika maeneo ya Kilwa,

Nako ngazi ya Halmashauri kumejitokeza wimbi la wanasiasa kutishwa na wengine kurubuniwa kwa fedha ili kuachia nafasi wanazoziwania kama ilivyoelezwa na Katibu wa Chama cha ACT Wazalendo Lindi Mjini Ahmad Machupa alipozungumza na Mashujaa FM kwa njia ya simu.

Aidha ameeleza kuwa, Chama cha ACT kimesimamisha wagombea katika mitaa yote 117 Lindi Mjini huku wagombea 6 wakijiondoa katika mchuano hali inayohusishwa na matukio ya rushwa huku mgombea 1 hajarudisha form baada ya kutishiwa uhai.

Pamoja na hilo MACHUPA amesema katika chama chake, wanawake na Vijana ndio waliojitokeza zaidi kuwania nafasi za uongozi na amewasihi wananchi kujitokeza katika zoezi la kupiga kura ifikapo Novemba 27, 2024 ili kuchagua viongozi sahihi watakaowaletea maendeleo.


Post a Comment

Previous Post Next Post