Baadhi ya Watumishi kutoka Wizara ya Afya, Ofisi ya Rais TAMISEMI wakiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi Msaidizi Sehemu ya Elimu ya Afya kwa Umma Dkt. Ona Machangu pamoja na baadhi ya wadau katika Kikao cha Ushirikiano na Wadau wanaotekeleza  Afua mbalimbali za Afya , Lishe na Ustawi wa Jamii kinachoratibiwa na Wizara ya Afya, kwa Kushirikiana na Ofisi ya Rais-TAMISEMI pamoja na wadau ikiwemo PACT  Tanzania kupitia Mradi wa ACHIEVE  Mkoani Arusha tarehe 24,Septemba 2024.

Mkurugenzi Msaidizi Sehemu ya Elimu ya Afya kwa Umma kutoka Wizara ya Afya  Dkt. Ona Machangu amesema Wahudumu wa Afya Ngazi ya Jamii wamekuwa na Mchango mkubwa katika utekelezaji wa Mipango  mbalimbali ya Afya ikiwemo Mpango wa Taifa wa Wahudumu wa Afya Ngazi ya Jamii, Mpango wa Taifa wa Malaria, Mpango wa Taifa wa Kudhibiti UKIMWI na Mpango wa Taifa wa Maonjwa Yalisiyopewa Kipaumbele. 

Mkurugenzi Msaidizi Sehemu ya Elimu ya Afya kwa Umma Dkt. Ona Machangu akizungumza katika Kikao cha Ushirikiano na Wadau wanaotekeleza  Afua mbalimbali za Afya , Lishe na Ustawi wa Jamii kinachoratibiwa na Wizara ya Afya, kwa Kushirikiana na Ofisi ya Rais-TAMISEMI pamoja na wadau ikiwemo PACT  Tanzania kupitia Mradi wa ACHIEVE  Mkoani Arusha tarehe 24,Septemba 2024.

Na. Elimu ya Afya kwa Umma 

Dkt. Machangu amebainisha hayo leo Septemba 24, 2024 Jijini Arusha katika Ufunguzi wa Kikao cha Ushirikiano na Wadau wanaotekeleza  Afua mbalimbali za Afya , Lishe na Ustawi wa Jamii kinachoratibiwa na Wizara ya Afya, kwa Kushirikiana na Ofisi ya Rais-TAMISEMI pamoja na wadau ikiwemo PACT  Tanzania kupitia Mradi wa ACHIEVE. 

Dkt. Ona amesema kuwepo kwa Wahudumu wa Afya Ngazi ya Jamii pamekuwa na mafanikio mengi katika afua za afya. “Pamekuwa na mafanikio makubwa sana uwepo wa CHW’s, kwenye Programu mbalimbali za HIV, Malaria, Kifua Kikuu na Programu nyinginezo nyingi “amesema Dkt. Machangu. 

Mratibu wa Huduma za Afya Ngazi ya Jamii kutoka Wizara ya Afya Dkt. Norman Jonas akizungumza katika Kikao cha Ushirikiano na Wadau wanaotekeleza  Afua mbalimbali za Afya , Lishe na Ustawi wa Jamii kinachoratibiwa na Wizara ya Afya, kwa Kushirikiana na Ofisi ya Rais-TAMISEMI pamoja na wadau ikiwemo PACT  Tanzania kupitia Mradi wa ACHIEVE  Mkoani Arusha tarehe 24,Septemba 2024.

Aidha, Dkt. Machangu amesema Mafunzo ya Wahudumu wa Afya Ngazi ya Jamii yatakayoanza tarehe 30, Septemba, 2024 yatasaidia kwa kiwango kikubwa katika kufanya kazi kwa ufanisi. 

Kwa upande wake Mratibu wa Huduma za Afya Ngazi ya Jamii kutoka Wizara ya Afya Dkt. Norman Jonas amesema Mpango Jumuishi wa Wahudumu wa Afya Ngazi ya Jamii utakuwa na mchango mkubwa kusogeza huduma karibu na mwananchi huku Afisa kutoka Mpango huo Dkt. Meshack Chinyuli akisema mikoa 10 ya kuanzia inatekeleza mpango huo. 

Kwa Upande wake Mratibu wa Huduma za Afya Ngazi ya Jamii kutoka Ofisi ya Rais TAMISEMI Dkt. May Alexander  amesema Mafunzo ya Wahudumu wa Afya Ngazi ya Jamii yatafanyika kwa miezi  sita ikiwemo miezi mitatu mafunzo nadharia na miezi mitatu mafunzo kwa vitendo(Field). 

Ikumbukwe kuwa Mpango Jumuishi wa Wahudumu wa Afya Ngazi ya Jamii ulizinduliwa rasmi Januari 31, 2024 na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Mpango ambapo Septemba 19, 2024 Waziri wa Afya Mhe. Jenista Mhagama alitangaza kuwa Mafunzo ya Wahudumu wa Afya Ngazi ya Jamii yataanza Septemba 30,2024 ambapo jumla ya Wahudumu wa Afya Ngazi ya Jamii 11,515 watapatiwa Mafunzo hayo na dhamira ya Serikali ni kufikia Wahudumu wa Afya Ngazi ya Jamii 137, 294 katika Mikoa yote ya Tanzania katika kipindi cha miaka mitano katika kufikia dhana ya afya kwa wote ifikapo mwaka 2030.

Post a Comment

Previous Post Next Post