Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora na Mbunge wa Kibakwe, George Simbachawene  ameishukuru na kuipongeza Wakala ya Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA)  kwa kuanza kujenga barabara za zege kwenye milima mikali iliyopo kata ya Mang’aliza-Kibakwe wilayani Mpwapwa.

Waziri Simbachawene ameyasema hayo wakati wa ziara  ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa miundombinu inayosimamiwa na TARURA  iliyofanywa na Naibu Katibu Mkuu wa OR-TAMISEMI anayeshughulikia miundombinu  Mhandisi Rogatus Mativila .

Post a Comment

Previous Post Next Post