Rais Joseph Boakai ametangaza atapunguza mshahara wake kwa Asilimia 40 huku Ofisi yake ikieleza ni sehemu ya kuonesha Utawala Unaowajibika

Hivi karibuni Wananchi wengi wamelalamikia kupanda kwa gharama ya maisha Nchini hapo ambapo Kituo cha BBC kimedai takriban Mtu mmoja kati ya Watano anaishi kwa chini ya Dola 2 (Tsh. 5200) kwa siku

Februari 2024, Boakai alisema mshahara wake wa Mwaka ulikuwa Dola 13,400 (Tsh. Milioni 35) na kuwa punguzo litamfanya iwe Dola 8,000 (Tsh. Milioni 20)

Wakati huo huo Wachambuzi wa Kisiasa wanadai kufanya hivyo hakuwezi kusaidia kwa kuwa anapata posho kila siku, pia Bajeti ya Ofisi ya Rais ni karibu Dola Milioni 3 (Tsh. Bilioni 7.8) kwa mwaka 2024


Post a Comment

Previous Post Next Post