Askari Polisi Wanne wa Kitengo cha Usalama Barabarani Wilaya ya Mwanga, waliokuwa wanashikiliwa kwa uchunguzi wamefukuzwa kazi baada ya kubainika wamefuta picha kwenye kamera za Jeshi la Polisi walizotumia kupima Mwendokasi (speed radar) wa Madereva kwa maslahi yao binafsi.

Taarifa hiyo imetolewa na Msemaji wa Jeshi la Polisi, DCP David Misime, pasipo kutaja Majina ya Askari hao huku akieleza walishtakiwa Kijeshi na wakapatikana na hatia ndipo Julai 8,2024 walifukuzwa kazi na kufutwa Jeshini

Post a Comment

Previous Post Next Post