Moto Wateketeza Zaidi ya Vibanda 300 vya Wafanyabiashara  Soko Kuu la Wilaya ya Masasi.


Vibanda 356 vikiwemo 256 vya wafanya biashara wadogo wadogo pamoja  vizimba 80 vya samaki na vibanda vya  mamalishe 20 vimeteketea kwa moto katika soko kuu la wilaya ya Masasi  maarufu soko la Mkuti hapa mkoani Mtwara. 

Tukio hilo limetokea usiku wa jana Julai 16,2024, kuamkia leo, hata hivyo mpaka sasa chanzo chake bado hakijajulikana ambapo kwa mujibu wa taarifa ya mkuu wa wilaya hiyo Lauteri Kanoni hakuna vifo wala majeruhi waliopatikana kutokana na moto.

Hii ni mara ya pili moto kuteketeza soko hilo ambapo June 2015 soko hilo liliteketea kwa moto na kupelekea vibanda zaidi ya 400 vya wafanyabiashara kuungua moto.

Post a Comment

Previous Post Next Post