Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Bw. Elijah Mwandumbya ametembelea Banda la Wizara ya Fedha katika Maonesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba) yanayofanyika katika viwanja vya Julius Nyerere Barabara ya Kilwa, Temeke, jijini Dar es Salaam, ambapo amepongeza mikakati iliyowekwa ya kutoa elimu kwa umma kuhusu majukumu ya Wizara na Taasisi zake.


Bw. Mwandumbya alisema kuwa Wizara ya Fedha ni Wizara muhimu katika kuchochea maendeleo ya mchi hivyo ni muhimu elimu ikatolewa kwa usahihi na ufanisi ili watanzania waweze kuelewa majukumu ya Wizara na Taasisi zake.

Amesema kuwa Maonesho hayo ambayo Idara, Vitengo na Taasisi za Wizara ya Fedha kwa pamoja zinatoa nafasi kwa watanzania kupata elimu kwa urahisi kuhusu Wizara hiyo.

Bw. Mwandumbya amewataka Wananchi kutembelea Banda la Wizara hiyo ili wapate elimu na huduma za kibenki, mifuko ya dhamana ya uwekezaji, Sera, masuala ya sekta ya fedha, usuluhishi wa masuala ya kodi, vyuo vya elimu ya juu, ununuzi na ugavi, pensheni na mirathi.

Post a Comment

Previous Post Next Post