Picha kwenye televisheni nchini humo ziliwaonyesha watu wakitumia kamba kuopoa magunia yaliyokuwa na mabaki ya miili ya binadamu kutoka kwenye maji yaliyojaa taka katika jalala la  Timbo huko Mukuru.

Kamanda Mkuu wa jeshi la polisi Kenya aliyejiuzulu, Japhet Koome


"Huku uchunguzi wa polisi ukiendelea, IPOA kwa uangalifu inafanya uchunguzi wa awali kubaini kama kulikuwa na uhusikaji wowote wa polisi katika vifo hivyo, au kushindwa kuchukua hatua kuvizuia," mamlaka hiyo ilisema.

Kurugenzi ya uchunguzi wa makosa ya jinai imesema uchunguzi unapendekeza wahanga wote waliuwawa kutumia mfumo sawa, bila kutoa maelezo.

Ofisi ya muendesha mashitaka ya umma pia iliangazia eneo ilipopatikana miili hiyo kuwa karibu sana na kituo cha polisi na kusema ina wasiwasi mkubwa kuhusu ugunduzi huo unaoashiria "ukiukaji mkubwa wa haki za binadamu".

Imeelekeza polisi iwasilishe matokeo ya uchunguzi wao katika kipindi cha siku 21, na pia kuzihimiza wakala za dola ikiwemo mamlaka huru ya IPOA kufanya uchunguzi kuhusu ripoti za watu kupotezwa kwa kutumia nguvu na vifo vinavyodaiwa kufanywa na polisi.

Tume ya haki za binadamu ya Kenya, asasi isiyo ya kiserikali, ilisema ilikuwa pia inahimiza uchunguzi wa kina ufanyike kubaini chanzo cha vifo hivyo na kuwatambua waliohusika.

(AFP)

Post a Comment

Previous Post Next Post