Kamati ya Kuduma ya Bunge ya Bajeti imesema serikali ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imelenga kuibua fursa za kiuchumi katika jamii kupitia miradi ya kilimo cha umwagiliaji kwa kujenga mabwawa, kukarabati skimu na kujenga skimu mpya za umwagiliaji za kimkakati kwa lengo la kuhakikisha taifa linakuwa na usalama wa chakula na kuwa na kilimo cha uhakika kwa zaidi ya msimu mmoja.

 


NIRC Dodoma.

Akizungumza na wananchi wakati wa ziara ya kamati hiyo kukagua miradi ya umwagiliaji ikiwemo bwawa la umwagiliaji la Membe wilayani Chamwino mkoani DODOMA, makamu mwenyekiti wa kamati hiyo Mhe, OMARI MOHAMED amewaasa wananchi wa Membe na vijiji jirani vitakavyonufaika na mradi huo kuunga mkono jitihada za serikali na kuwa tayari kuchangamkia fursa zitakazojitokeza katika mradi huo ikiwemo kulima zaidi ya mara moja kwa mwaka, shughuli za uvuvi na fursa nyinginezo za kiuchumi zitakazoibuka kupitia uwepo wa bwawa hilo la umwagiliaji katika maeneo yao.

Kwa upande wake Naibu waziri wa Kilimo Mhe, David Silinde amesema Wizara ya kilimo itaendelea kusimamia miradi yote ya umwagiliaji kwa karibu na umakini ili kuhakikisha inakamilika kwa wakati na viwango vya ubora unaotakiwa na kuleta tija kwa wananchi na hatimae kufikia malengo ya agenda 1030.

Naye, Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya umwagiliaji Bw, RAYMOND MNDOLWA amesema ziara ya wajumbe wa  kamati ya bunge ya Bajeti imelenga kukagua miradi  8 ya umwagiliaji inayotekelezwa na Tume katika baadhi ya mikoa ambapo katika mkoa wa Dodoma imetembelea mradi wa ujenzi bwawa la Membe pamoja na mradi wa mashamba makubwa (Block Farms) Chinangali kwa ajili ya vijana kupitia mradi wa Jenga Kesho iliyo bora BBT, ambapo kamati hiyo imekagua ujenzi wa nyumba za makazi kwa ajili ya vijana wanufaika wa mradi huo pamoja na eneo litakapochimbwa bwawa kwa aajili ya ajili ya kilimo cha umwagiliaji.

Kukamilika kwa bwawa la Membe litakuwa na uwezo wa kuhifadhi maji lita bilioni 12 za ujazo mara litakapokamilika ambapo linajengwa kwa gharama ya zaidi Shilingi  Bilioni 12 na linatarajiwa kukamilika Februari mwaka 2024.

Post a Comment

Previous Post Next Post