Anamringi Macha ameteuliwa na vikao vya chama cha Mapinduzi kuwa Naibu Katibu Mkuu Bara jana Novemba 29, 2023 akichukua nafasi ya Christian Mndeme.

Mwezi July 2023 Anamringi aliteuliwa na aliyekuwa Rais wa awamu ya tano Hayati Dkt. John Pombe Magufuli kuwa mkuu wa wilaya ya Kahama na kuchukua nafasi ya Fadhili Nkurlu ambaye uteuzi wake ulitenguliwa.

Itakumbukwa January 20, 2020 akiwa mkuu wa wilaya, Anamringi Macha aling’ara katika vichwa vya habari baada ya kuonekana akigawa ndizi na mahindi ya kuchemsha kwa Wananchi waliopanga foleni kufuatilia namba za NIDA ili waweze kusajili laini zao kwa alama za vidole na kuepuka kufungiwa kutokana na tangazo lililotolewa na TCRA.

Macha amewahi kuwa mkuu wa mkoa wa Shinyanga, katibu msaidizi wa CCM kuanzia ngazi za wilaya na baadaye akashikilia nafasi hiyo katika ngazi ya mkoa. Aidha amewahi kuwa katibu msaidizi mkuu idara ya uenezi na katibu wa sekretarieti.

Post a Comment

Previous Post Next Post