Naibu Waziri wa Nishati, Mhe. Judith Kapinga amewataka
wananchi kuhakikisha wanalinda na kutunza miundombinu ya umeme nchini
ili itumike kwa muda mrefu.
Amesema
hayo tarehe 29 Novemba, 2023 mkoani Morogoro wakati akiwasha umeme kwa
mara ya kwanza katika Vijiji vya Maseyu na Newland vilivyopo katika Kata
ya Gwata na alipofanya ziara ya kukagua utejekezaji wa Miradi ya
kusambaza Umeme Vijijini inayoratibiwa na Wakala wa Nishati Vijijini
(REA) mkoani humo.
Amesema
serikali imekuwa ikitumia fedha nyingi katika Utekelezaji wa Miradi ya
Kusambaza Umeme Vijijini kwa lengo la kuharakisha maendeleo kwa
Wananchi, hivyo wanapaswa kusaidia kulinda miundimbinu hiyo ili
iwanufaishe wananchi wengi na kwa muda mrefu.
“Msiruhusu
upenyo wa mtu yeyote kuhujumu miundombinu, tuhakikishe tunailinda
kwani serikali imewekeza fedha nyingi na tuipe thamani inayostahili",
amesema Naibu Waziri Kapinga.
Amesema
serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dkt. SamiaSuluhu Hassan
imejipambanua kwa kuwaletea wananchi maendeleo kwa kuweka miundombinu
wezweshi ili waweze kushiriki shughuli mbali mbali za uchumi.
Serikali
ya Awamu wa Sita ni ya maendeleo hivyo wananchi wanapaswa kutumia
huduma ya upatikanaji wa umeme vijijini kujiinua kiuchumi kwa kuutimia
katika shughulli za biashara.
Naibu
Waziri Kapinga amewataka wakandarasi wanaojenga miradi ya REA
kuhakikisha wanaikamilisha kwa wakati ili ifikapo Juni 2024 miradiyote
iwe imekamilika.
Akielezea
utekelezaji wa miradi, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa REA, Mhandisi Jones
Olotu amesema Serikali imewekeza jumla ya shilling 114.6 Billioni kwa
miradi mitano inayotekelezwa kwa Mkoa wa Morogoro.
Amesema
Serikali kupitia REA inaendelea kutekeleza miradi mbalimbali nchi nzima
pamoja na kuwasimamia kwa karibu wakandarasi wote waliopewa zabuni
yakutekeleza miradi mbalimbali ya umeme ili kuhakikisha miradi hiyo
inakamilika kwa wakati na kwa ubora unaotakiwa.
Mhandisi
Olotu amesema Mkoa wa Morogoro una jumla ya vijiji 669 ambapo hadi
kufikia sasa vijiji 583 sawa na asilimia 87.1% vimepata huduma ya umeme
kupitia mitano.
Ameitaja
miradi hiyo kuwa ni REA Awamu ya Tatu Mzunguko wa Pili (REA III Round
II), Mradi wa Kituo cha Kupoozea Umeme cha Ifakara, Mradi wa ujazilizi
(Densification IIB), Mradi wa Kupeleka umeme kwenye migodimidogo na
maeneo ya kilimo na Mradi wa Kupeleka umeme kwenye Vituo vya Afya na
Pampu za Maji.
Kwa upande
wake, Mbunge wa Morogoro Kusini Mashariki, Mhe. KhamisTaletale
aliishukuru Serikali kwa utekelezaji wa kutoa fedha za kutosha kwa ajili
ya utekelezaji wa miradi ya Nishati Vijijini Jimboni Kwake.
Post a Comment