YOUR FUTURE IS CREATED BY WHAT YOU DO TODAY, NEVER TOMORROW

Kutokana mazoezi kuwa na umuhimu mkubwa katika mwili wa binadamu ikiwemo kuboresha afya ya ngozi,kuzuia magonjwa yasiyo ya kuambukiza kama vile mshituko wa moyo na kisukari, kudhibiti uzito wa mwili, mifupa kuwa na nguvu na kuboresha afya ya mwili, Waandishi wa Habari  mkoa wa Dodoma  wameanzisha mpango kwa kufanya mazoezi mbalimbali ya mwili nyakati za jioni mara baada ya saa za kazi.


Na.Elimu ya Afya kwa Umma.

Hiyo ni katika kuunga kuunga mkono jitihada za Wizara ya Afya ,Elimu ya afya kwa Umma za uhamasishaji jamii umuhimu wa mazoezi ili kuepuka magonjwa yasiyo ya kuambukiza.

Akizungumza katika uwanja wa shule ya Sekondari Dodoma Katibu  Msaidizi wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Dodoma Fred Alfred  ambaye pia ni mwandishi wa Habari kutoka gazeti la Uhuru amesema wameamua kufanya hivyo katika kuunga mkono juhudi za Serikali ya awamu ya Sita chini ya Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kupitia Wizara ya Afya, Elimu ya Afya kwa Umma za kupambana na Magonjwa yasiyo ya Kuambukiza.

“Program hii ni katika kuunga juhudi za serikali katika kuepuka magonjwa yasiyo ya kuambukiza  nitoe wito kwa wanahabari na jamii kwa ujumla  tujitokeze kufanya mazoezi tuimarishe afya zetu“amesema.

Kwa upande wao baadhi ya Waandishi wa Habari akiwemo Daniel Mkate kutoka EATV  amesema ni muhimu kuwa mabalozi wazuri wa vitendo na si kwa kuandika Habari pekee katika kuhamasisha jamii umuhimu wa mazoezi huku  Ramadhan Hassan kutoka gazeti la Mwananchi akisema  atahakikisha anapiga chini kitambi kwa kufanya mazoezi.

“Tumekuwa hodari wa kuhamasisha wengine kupitia kalamu zetu hivyo nawaomba wanahabari wengine hasa wakongwe wenzangu tujitokeze tufanye mazoezi” amesema Daniel Mkate kutoka EATV .

“Tupige chini kitambi, tupige chini unene usiokuwa na tija, tuiweke vizuri miili yetu ili kuhakikisha mambo yanakuwa vizuri na nina hakika kwa mazoezi haya uwezo wetu wa kuandika stori utaongezeka”amesema Ramadhan Hassan kutoka gazeti la Mwananchi.

Post a Comment

Previous Post Next Post