Wananchi wa Wilaya ya Lindi wamesema ujenzi wa Barabara kwenye baadhi ya maeneo ya Wilaya hiyo utarahisisha usafirishaji wa abiria na mazao yao na kuwawezesha kuyafikia maeneo yenye huduma muhimu kama hospitali, masoko na shule.  


Wakazi hao ni kutoka Nyangao ambako kuna Ujenzi wa barabara ya Mahiwa-Namangale, Nyengedi kwenye ujenzi wa barabara ya Nyengedi, mnara hadi Rondo forest km 5 kwa kiwango cha lami na Nangaru kunakojengwa barabara hadi Milola kwa kiwango cha changarawe.  

Wameeleza hayo wakati  wa ziara ya Mkuu wa Wilaya ya Lindi Shaibu Ndemanga na kamati ya ulinzi na usalama na waliyotetembelea miradi 7 ya barabara inayojengwa wilayani humo sambamba na kivuko 1 kilichopo Kijiji cha Mchinga ambacho ujenzi wake umekamilika.  


Wakati wa ziara hiyo, Meneja wa TARURA Wilaya ya Lindi Mhandisi Dawson Paschal amesema thamani ya miradi yote 7 ni shilingi Bilioni 5.7 na kati ya hiyo, barabara km 5.7 inajengwa kwa kiwango cha lami.  


Pia amezitaka halmashauri kupima barabara zenye upana wa kutosha ili kuondoa changamoto wanazokutana nazo wakati wa ujenzi ikiwemo kuwepo kwa upana mdogo.  Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Lindi Shaibu Ndemanga amewasisitiza TARURA kuwasimamia wakandarasi wajenge kwa ubora.

Post a Comment

Previous Post Next Post