YOUR FUTURE IS CREATED BY WHAT YOU DO TODAY, NEVER TOMORROW

Mahakama ya Wilaya ya Kilwa imewatia hatiani Maafisa Forodha wa TRA Wilayani humo, SULTAN ALI NASOR na SILVER MAXIMILLIAN kwa makosa ya Matumizi Mabaya ya madaraka na kutofanya Tathmini Sahihi ya Kodi iliyosababishia Mamlaka Hasara ya Tsh. Milioni 9.269. 


Washtakiwa walifanya tathmini ya kodi kwa madumu ya mafuta ya kupikia 200 tu badala ya 500 ya lita 20 kila moja, yaliyoingizwa kutoka Zanzibar, mali ya Mfanyabiashara ATHUMANI AHMADI SIMBA.  

Simba alishtakiwa kwa kushindwa kulipa kodi ambapo alikiri kosa na kulipa Tsh. 9,269,066.38/-, huku Washtakiwa wengine wakihukumiwa Miaka 3 jela kwa kosa la kwanza na la pili kila mmoja au kulipa faini ya Tsh. 250,000/= kila mmoja kwa kila kosa, na kifungo cha nje mwaka 1 kila mmoja kwa kosa la 3.

Post a Comment

Previous Post Next Post