YOUR FUTURE IS CREATED BY WHAT YOU DO TODAY, NEVER TOMORROW
Padri Kitima ameishauri serikali iunde kampuni itakayosaini mkataba wa uboreshwaji na uendeshaji wa Bandari kati yake na Serikali ya Dubai (The Emirates of Dubai)
Ushauri huo umetolewa baada ya kikao cha Viongozi wa dini mbalimbali waliokutana na Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa kujadili Mkataba wa Bandari kati ya Serikali ya #Tanzania na Kampuni ya #DPWorld
Akizungumza kwa niaba ya Viongozi hao, Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (#TEC), Padri Charles Kitima amesema “Serikali inatakiwa kuunda Kampuni ambayo hata ikitokea migogoro inayoshtakiwa ni Kampuni na sio Nchi.”
Amesema “Wenzetu wameunda Kampuni badala ya Serikali kujimwaga moja kwa moja, ndicho walichofanya #Dubai, hata inaposhtakiwa inakuwa ni Kampuni badala ya Nchi. Mfano inatokea unamnyang’anya Mtu Ekari 10 anaenda kushikilia Ndege ya mabilioni.”
Post a Comment