YOUR FUTURE IS CREATED BY WHAT YOU DO TODAY, NEVER TOMORROW

Mratibu wa dawati la jinsia na Watoto mkoa wa Lindi ambaye ni mkaguzi msaidizi wa jeshi la polisi Joyce Kitesho amesema amani isipokuwepo kwenye familia waathirika wakubwa huwa ni Watoto. 

Mkaguzi Msaidizi wa Jeshi la Polisi Joyce Kitesho (Picha na Edna Kahema)


Kitesho ameyasema hayo leo Mei 24, 2023 alipokuwa anazungumza katika kipindi cha Kuchele kinachorushwa na Mashujaa FM kuhusu siku ya wanawake kimataifa kwa amani na upokonyaji silaha ambapo ameeleza kuwa, ni jukumu la kila mmoja hasa mwanamke kuhakikisha hakuna mtu yeyote anaivuruga amani kuangazia katika ngazi ya familia mpaka kitaifa. 

Aidha Kitesho ameeleza kuwa, kukosekana kwa amani huleta madhara mengi ikiwemo vifo, ukatili wa kingono, njaa, msongo wa mawazo, majeraha n.k 

Akizungumzia kuhusu maadhimisho ya siku hiyo msaidizi wa jeshi la polisi upande wa dawati la jinsia mkoa wa Lindi Frida Muhangilwa amesema ni vyema jamii ikatambua vurugu sio njia ya kutatua changamoto ambazo zinatokea kwani changamoto hizo hutatuliwa kwa njia ya mazungumzo.

Post a Comment

Previous Post Next Post