Wafanyabiashara mkoa wa Lindi wamelalamikia utitili wa kodi na mamlaka makubwa aliyopewa Mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) ikiwemo kufungia ‘account’ za fedha za wafanyabiashara wanaposhindwa kulipa tozo mbalimbali ama kufikia makubaliano na mamlaka hiyo suala ambalo limekuwa likirudisha nyuma maendeleo yao.

Yamezungumzwa hayo katika kikao cha Wafanyabiashara kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano ofisi ya mkuu wa mkoa wa Lindi leo tarehe 30 Mei, 2023 na kuongozwa na Mwenyekiti wa kamati iliyoundwa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ili kukusanya maoni na kero za wafanyabiashara nchini.


Wafanyabiashara wakiwasilisha maoni na kero zao 

Aidha wameomba kuundwa utaratibu na kanuni zitakazoutambua mkoa wa Lindi kwa changamoto zake ukilinganishwa na mikoa iliyopiga hatua kimaendeleo ikiwemo Mbeya, Dar es Salaam na Arusha.

Katibu Tawala Msaidizi mkoa wa Lindi idara ya Biashara, Viwanda na uwekezaji Dkt. Bora Haule

Katibu Tawala Msaidizi mkoa wa Lindi idara ya Biashara, Viwanda na uwekezaji Dkt. Bora Haule amewahakikishia wafanyabiashara mazingira mazuri na fursa zaidi za uwekezaji na kuwaomba kutokata tamaa kutokana na changamoto wanazokumbana nazo kwani serikali ya mkoa inaendelea kuzifanyia kazi.

 Mwenyekiti wa jumuiya ya wafanyabiashara taifa Hamis Livembe ambaye pia ni mwenyekiti mwenza wa kamati ya Waziri Mkuu

Mwenyekiti wa jumuiya ya wafanyabiashara taifa Hamis Livembe ambaye pia ni mwenyekiti mwenza wa kamati ya Waziri Mkuu iliyoundwa kwa lengo la kukusanya maoni na kero za wafanyabiashara kote nchini amewaomba wafanyabiashara mkoa wa Lindi kuwa na imani na kamati hiyo na ameahidi kuzifanyia kazi changamoto zote walizoziwasilisha na kuzifikisha mahali husika kwa hatua zaidi.

Wafanyabiashara waliohudhuria mkutano

Post a Comment

Previous Post Next Post