Kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru kitaifa Abdallah Shaib Kaim leo April 12, 2023 ameweka jiwe la msingi katika Ujenzi wa mabweni ya wasichana Katika shule ya Sekondari ya wasichana ya Lucas Malia Wilayani Ruangwa ili kuhakikisha mtoto wa kike anapata Elimu bila kukatishwa ndoto zake. Mradi huo unagharimu kiasi cha shilingi millioni 200.

Kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru kitaifa Abdallah Shaib Kaim (Kulia) akizindua jiwe la msingi la mradi wa ujenzi wa mabweni 2 shule ya wasichana ya Lucas Malia Wilayani Ruangwa akiwa na Mkuu wa Wilaya ya Ruangwa Hassan Ngoma (wa tatu kushoto)

Akizungumza Wakati wa uwekaji wa jiwe la msingi kwenye mradi huo, kiongozi huyo wa mbio za mwenge 2023 amehamasisha wahandisi nchi nzima kufanya kazi kwa uzalendo wakitanguliza maslahi ya wananchi na Taifa kwa ujumla na kuachana na tabia ya kufanya kazi pale tu wanapoona viongozi wanakuja kwenye miradi.


Kwa upande wake mkuu wa Wilaya ya Ruangwa Hassan Ngoma ameeleza kuwa, ujenzi wa mradi huo ni mkombozi kwa wanafunzi wa kike ambao wengi wao wamekuwa wakikutana na changamoto ambazo wakati mwingine zinadidimiza ndoto zao.

Mkuu wa Wilaya ya Ruangwa Hassan Ngoma (wa pili kulia) akipokea Mwenge wa Uhuru kutoka kwa Mkuu wa wilaya ya Lindi Shaibu Ndemanga

Aidha ameahidi kuwa, mazingira ya mabweni hayo  yatatunzwa vizuri ikiwa ni pamoja na kuendeleza upandaji wa miti kama kauli mbiu ya mwenge kwa mwaka 2023 inavyohamasisha utunzaji wa mazingira.

Post a Comment

Previous Post Next Post