Jeshi la Polisi Mkoani Lindi linamshikilia Shabani Saidi Makota (20) mkazi wa Likongowele Wilayani Liwale Mkoani humo kwa tuhuma za mauaji ya Siamini Rashidi Mkong’ondo (40) mkazi wa Likongowele kwa kumkata na panga kichwani.


Na Elizabeth Msagula

Tukio hilo limetokea katika kijiji cha Nganyaga kata ya Likongowele februari 5,2023.

Kamanda wa polisi Mkoa wa Lindi, Kamishna msaidizi wa polisi Pili Mande amethibitisha kutokea kwa tukio hilo akisema chanzo cha mauaji hayo ni kudaiana fedha ya pango na fedha ya malipo ya kubangua korosho.

Aidha ameeleza kuwa, mtuhumiwa alikuwa ni mpangaji katika nyumba ya marehemu, aliyempa ujira wa kubangua korosho kwa malipo ya shilingi elfu kumi tangu tarehe 3 na hakumlipa. 

Ndipo mtuhumiwa akaanza kudai wakati huo naye marehemu akaanza kumdai mtuhumiwa fedha ya pango na baadae alimfungia mtuhumiwa ndani ya chumba alichopanga ili asitoke hadi afike kiongozi wa kitongoji lakini mtuhumiwa alifanikiwa kuvunja mlango na kutoka na panga alilojeruhi nalo marehemu kichwani na kupelekea kifo chake.

Amesema baada ya mwili wa marehemu Mkong’ondo kufanyiwa uchunguzi katika hospitali ya Wilaya ya Liwale imebainika kuwa, kifo chake  kimetokana na kuvuja damu nyingi na kukosa hewa.

Post a Comment

Previous Post Next Post