YOUR FUTURE IS CREATED BY WHAT YOU DO TODAY, NEVER TOMORROW

Mzee Joseph, Baba mzazi wa marehemu

Na Mwandishi Wetu

Watu wawili wa familia moja wameuwawa na watatu kujeruhiwa katika kijiji cha Nammanga wilayani Nachingwea mara baada ya kijana mmoja anayefahamika kwa jina la John Barnaba 48 Kuwashambulia kwa kuwapiga na kitu kizito kichwani kinachodhaniwa kuwa ni mpini wa shoka.

Dada wa marehemu Bonifasia Joseph ameeleza kuwa waliouawa ni Joseph Joseph 41 na Mendradi Joseph 46 ambao walifika nyumbani kwa Dada yao kwaajili ya kumsaidia wakati alipokuwa akizozana na mtuhumiwa John Barnaba.

Baadae mabishano yakapelekea ugomvi na kusababisha vifo. Pia mtuhumiwa huyo amesababisha majeraha kwa Baba Mzazi wa vijana hao ambaye amevunjwa mkono pamoja na ndugu wengine.

Kwa upande wake mwenyekiti wa kitongoji hicho, Dua Hokororo ameeleza kuwa, tukio hilo limetokea majira ya saa tatu usiku ambapo mara baada ya mtumiwa kufanya tukio hilo walifanya jitihada za kumkamata na kumfikisha katika ofisi ya kata ya Ruponda kwa usalama zaidi na baadae walitoa taarifa polisi ambao wamefika katika eneo la tukio na baada ya uchunguzi wanafamilia wameruhusiwa kuendelea na taratibu za mazishi.

Mkuu wa upelelezi wilayani humo akizungumza na wananchi amekemea matumizi ya pombe kupita kiasi pamoja na uvutaji wa bangi kwani baada ya mahojiano ya awali na mtuhumiwa huyo amekiri kutumia pombe aina ya Gongo pamoja na Bangi. Jeshi la polisi linaendelea na uchunguzi zaidi ili kumfikisha mtuhumiwa mahakamani.

Post a Comment

Previous Post Next Post