Pele, gwiji wa soka na
mchezaji wa timu ya taifa ya Brazil aliyekulia kwenye umaskini na hatimaye kuwa
mmoja wa wanamichezo wakubwa duniani, amefariki jana Alhamisi akiwa na umri wa
miaka 82.
Taarifa ya Hospitali ya
Albert Einstein iliyoko mjini Sao Paulo, ambako Pele alikuwa akipokea matibabu,
imesema gwiji huyo wa kandanda alifariki saa tisa na dakika 27 alasiri kutokana
na viungo vyake kushindwa kufanya kazi.
Pele alikuwa akiugua saratani
ya utumbo.
Kifo cha Pele, ambaye ni
mchezaji pekee aliyeshinda Kombe la Dunia la FIFA mara tatu mwaka 1958, 1962 na
mwaka 1970, kilithibitishwa kupitia akaunti yake ya mtandao wa Instagram kwa
taarifa iliyoandikwa;
"Msukumo na upendo ndio
sifa zilizopamba safari ya Mfalme Pele, aliyefariki dunia leo," Na kuongeza
"aliiletea dunia furaha kutokana na kipaji chake katika soka, alizuia
vita, alifanya kazi za kijamii duniani kote na kueneza kile alichoamini kuwa
tiba ya matatizo yetu yote: upendo."
Salamu za rambi rambi
zinaendelea kumiminika kutoka kile pembe ya dunia- kutoka kwa watu maarufu
katika fani ya michezo, siasa, burudani, sanaa na tamaduni, kwa mtu maarufu
aliyeiweka Brazil katika ramani ya soka duniani.
Hakika atakumbukwa kwa alama
ya ubora aliyoiacha katika ulimwengu wa soka.
Post a Comment