YOUR FUTURE IS CREATED BY WHAT YOU DO TODAY, NEVER TOMORROW


Na Kweli Emcee

Mwanaume  moja kutoka nchini Zimbabwe anayefahamika kwa jina la Vashko Sande amewashangaza watu baada ya kumuoa mama mkwe wake kama mke wa pili ambaye alichumbiana naye kwa siri kwa miaka 7, anasema yeye ni baba mkwe wake mwenyewe.

Vashko Sande alifanya jambo lisilofikirika alipompenda mama-mkwe wake, akimsaliti na kuvunja uaminifu wa mke wake.

Inasemekana kuwa aligeuka na kuwa mnyanyasaji baada ya kupata mapenzi mapya na hata wazee walishindwa "kumtia adabu" kwani alikaidi kanuni za kijamii na kumwoa mwanamke huyo kama mke wake wa pili.

Mke wake aitwaye Vimbai Magora, alishindwa kukubaliana na tabia ya unyanyasaji ya mumewe na ilimlazimu kutafuta msaada wa sheria.

Magora katika ombi lake la kutaka amani alisema: “Tulifunga ndoa mwaka 2008 na tangu 2011 mume wangu mara nyingi alijawa na chuki kwani alikuwa amempenda mama yangu.

"Alianza kunipiga na kunitusi, akitishia kunifukuza mimi na watoto wangu wanne katika nyumba yetu tuliyoiandaa wote kipindi chote cha ndoa."

Aidha alifichua kuwa, hata wazee wa familia walishindwa kutatua tatizo lao kwani hakuwahi kusikiliza ushauri wao, bali aliendelea na uhusiano na mama mkwe wake akiweka ndoa yao juu ya mawe.

Akijibu, Sande alithibitisha madai yaliyoelekezwa kwake akisema aliwapenda wanawake hao wawili na alitaka kutumia maisha yake yote pamoja nao.

“Ni kweli ninampenda mama yake, lakini bado nampenda mke wangu pia. Kwa hiyo, ningependa kukaa nao maisha yangu yote,” 

Hakimu wa mahakama ya Zvishavane Shepherd Mjanja alitoa amri hiyo ya amani kwa upande wa Magora kwa kuamriwa asimnyanyase mke wake wa kwanza kimwili na kihisia.

Post a Comment

Previous Post Next Post