YOUR FUTURE IS CREATED BY WHAT YOU DO TODAY, NEVER TOMORROW

Kutoweka kwa mwandishi mpekuzi nchini Tanzania Azory Gwanda hatimaye kumechukua mwelekeo mpya baada ya waziri wa maswala ya kigeni nchini humo kusema kwamba mwandishi huyo 'alitoweka na kufariki'.

Image result for Azory Gwanda

Mwandishi huyo wa Tanzania alikuwa akiifanyia kazi kampuni ya Mwananchi wakati alipotekwa katika mazingira ya kutatanisha.

Alikuwa akiripoti kesi za mauaji ya kiholela katika eneo la kibiti katika mwezi uliopelekea kupotea kwake.

Serikali imedai kuchunguza kesi yake na za watu wengine waliotoweka lakini hakuna kilichoafikiwa hadi sasa.
Mjadala katika mitandao ya kijamii kuhusu kauli iliyotolewa sasa na waziri Palamagamba Kabudi imegusia maswali kama vile:
- Kipi cha kuaminiwa?
- Je ni vipi familia ya Gwanda itakavyoweza kupata ukweli na amani kuhusu kilichotokea?
-  Na kama Gwanda amefariki, nani aliyemuua na kaburi lake liko wapi?


Post a Comment

Previous Post Next Post