YOUR FUTURE IS CREATED BY WHAT YOU DO TODAY, NEVER TOMORROW
Sasa unaweza kuitazama video ya SIR ELLY_ ONDOA GIZA akiwashirikisha NARI MC ambaye amefanya verse ya pili, pamoja naye PRIME NUMBER ambaye ameshiriki verse ya pili.
VIDEO imetengenezwa na MAWEHU PICTURES ambao wamekuwa wakifanya vizuri katika uwasilishwaji wa kazi za wasanii wachanga na shughuli nyinginezo nyingi za kijamii. Wakati huo AUDIO imetengenezwa ndani ya studio za BOKAZI ENTERTAINMENT chini ya MAN DVD ambaye ndiye producer wa wimbo huo - ONDOA GIZA KITAA.
BOKAZI ENTERTAINMENT ni waandaaji wakongwe katika enzi yao ya MUZIKI HURU kutoka TANZANIA. Awali wakishirikiana na UYOGA BOGA VILLAGE waliweza kuzungumza mambo muhimu kwa jamii inayowazunguka kwa kutumia muziki hususani muziki wa HIP HOP juu ya matatizo na changamoto za maisha ya kila siku ya watu wakigusia misimamo mbalimbali ya SERIKALI na hata WADAU tofauti wa shughuli za kijamii wakilenga kudhihirisha bayana ama kweli ambayo imeonekana ama ilionekana wazi haina uwiano sawa wa kimaslahi kwa WATANZANIA WOTE.
FUATA LINK HAPA CHINI KUTAZAMA VIDEO - ONDOA GIZA KITAA:
LIKE | COMMENT | SHARE
Post a Comment