Shadrack Chaula (24) ameachiwa huru leo Julai 8, 2024 baada ya kulipa faini ya Tsh. Milioni 5 ikiwa ni siku chache tangu alipohukumiwa kifungo cha Miaka Miwili jela au kulipa Faini hiyo kwa kosa la kutoa taarifa za uongo Mtandaoni.

Chaula ambaye ni Msanii wa Sanaa ya Uchoraji, Julai 2, 2024 alionekana kupitia kipande cha video akichoma moto picha ya Rais Samia Suluhu Hassan, alihukumiwa na Mahakama ya Wilaya ya Rungwe Mkoa wa Mbeya, alishindwa kulipa faini na kwenda jela, Wadau mbalimbali walianza kumchangia fedha kupitia Mtandao kwa nia ya kumlipia faini

Wakili Michael Lugina amesema “Sisi Mawakili tumekuja kusimamia zoezi la kumlipia faini iliyochangwa na Wadau wa Mtandaoni, tayari ametoka na tumekamilisha mchakato lakini tunafanya taratibu nyingine za kukata rufaa kwa maana ya kupinga mwenendo wote wa kesi.”

C: JF

Post a Comment

Previous Post Next Post