Mganga mfawidhi wa hospitali ya wilaya ya Nachingwea Dk. Shukrani Msikini amewashukuru madaktari bingwa kwa kufika wilayani Nachingwea kwani wamesaidia wagonjwa wengi wenye uhitaji kupata tiba.

Akizungumza ofisini kwake, amesema madaktari wa hospitali ya wilaya hiyo pia wamepata faida kupitia program ya madaktari bingwa wa Samia kwani imewaiongezea ujuzi mbalimbali ambayo ni sehemu ya malengo makuu ya mpango wa serikali.

Aidha, Msikini amesema wananchi wengi walijitokeza kupata matibabu na wengi wao wamepona na wengine wanaendelea vizuri.

Sambamba na hayo amewataka wananchi kutumia vizuri fursa kama hiyo pindi inapotokea.


Post a Comment

Previous Post Next Post