Msafara wa Katibu wa NEC Itikadi Uenezi na Mafunzo wa CCM - Paul Makonda umepata ajali Masasi mkoani Mtwara.  



Ajali hiyo iliyotokea saa 9 alasiri imehusisha zaidi ya magari 7 yaliyokuwepo katika msafara huo uliokuwa unatoka mkoani Ruvuma kuelekea jijini Dar es salaam.  

Taarifa zilizothibitishwa kutoka eneo la tukio zinaeleza kuwa, watu wasiopungua 7 wamejeruhiwa na kukimbizwa katika hospitali ya mkoa wa Mtwara na hakuna kifo kilichoripotiwa.  

Taarifa zinaeleza kuwa, hali ya kiafya ya Paul Makonda ni salama.

Post a Comment

Previous Post Next Post