Kila inapofika  mwezi Januari kila mwaka Tanzania inaungana na Mataifa mengine duniani kuhamasisha huduma za uchunguzi wa Saratani ya mlango wa kizazi, akina Mama Wilayani Hanang Mkoani Manyara wamekuwa na mwitikio wa kuchunguza Saratani kutokana Elimu ya Afya inayotolewa. 


Na. Elimu ya Afya kwa Umma 

Katika uchunguzi huo, Jumla ya akina mama 228 wamechunguzwa Saratani ya Mlango wa kizazi Wilayani Hanang huku wito ukitolewa wananchi Kujenga tabia ya kuchunguza Afya mara Kwa  mara 

Aidha, akina  mama watatu wamegundulika kuwa na maambukizi  ambapo Mama mmoja alikuwa na saratani ya mlango wa kizazi na alipewa rufaa ya kwenda Hosipitali ya  Hydom Uchunguzi umefanyika katika vituo 40 kwa mkoa wa Manyara ,kwenye maeneo ya Hosipitali ,vituo vya afya pamoja na zahanati kama anavyoeleza Kaimu  Mganga mkuu wa mkoa Manyara.

Wizara ya afya kupitia idara ya afya ya uzazi mama na mtoto ikiambatana na wadau wa maendeleo Usaid Afya yangu Northern , imetumia fursa ya uhamasishaji  mwezi wa ugonjwa wa saratani ya mlango wa  kizazi kuwatia moyo wakazi wa Hanang waliokumbwa na maafa ya mafuriko Kwa kufikisha huduma hii karibu ya uchunguzi wa saratani ya mlango wa kizazi na saratani ya Matiti ,DKt Saphina Yuma  mratibu programu wa via vya uzazi wizara ya afya anafafanua

Miongoni mwa wakazi waliofanikiwa kupata huduma hiyo wameishukuru serikali KwA kufikisha huduma hiyo kwani wanaamini afya zao Zitakuwa salama

Post a Comment

Previous Post Next Post