Mpango wa Umoja wa Mataifa wa kutafuta ukweli umezitaka pande zote mbili nchini Sudan kusitisha mapigano.


Na Jacob Safari - DW

Mpango huo ulio na wanachama watatu umeanza kazi yake ya kuchunguza madai ya ukiukaji wa haki za binadamu katika mapigano hayo.

Kikosi hicho kimetoa wito kwa pande mbili zinazozozana katika mzozo huo kusimama na majukumu yao ya kuwalinda raia na kuhakikisha kwamba wachochezi wa matukio mabaya ya uhalifu wanachukuliwa hatua.

Wanachama wa kikosi hicho huru cha Umoja wa Mataifa waliteuliwa mnamo Disemba 18.

Mwenyekiti wa mpango huo ni Mohamed Chande Othman, ambaye ni jaji mkuu wa zamani wa Tanzania na atakuwa anashirikiana na Joy Ezeilo mkuu wa kitengo cha sheria katika chuo kikuu cha Nigeria na Mona Rishmawi aliye na uraia wa Jordan na Uswisi ambaye ni mtaalam huru wa zamani wa Umoja wa Mataifa kuhusiana na masuala ya haki za binadamu Somalia.

Post a Comment

Previous Post Next Post