ROMA MKATOLIKI na WAKAZI wameonekana kutokubaliana jambo na kukaa meza moja kufuatia mjadala unaoendelea kati yao kupitia mtandao wa X ukionesha wakali hao wa muziki katika miondoko ya Hip Hop kutoka nchini Tanzania kutopendezwa na maoni ya kila mmoja wao.

Baada ya ROMA kuandika "Huna bado nafasi ya kunishauri nitumie reply gani, mimi ndio nina maamuzi nitumie silaha gani kujibu!!" ...

... Bila shaka ujumbe huu ulielekezwa kwa WAKAZI ambaye yuko katika "Media Tour" aki-promote kazi yake mpya, naye akajibu;

"Ni sababu huwezi kwenye michano! acha kujitetea hapa!  Nipo media tour, naulizwa maswali najibu… Sikuhitaji kwa chochote! Acha kulialia and do something kama unakerwa na interview zangu ambazo zina expose ukweli na uhalisia wa mambo." Wakazi ameandika katika mtandao wa X.

Wakati tukijiuliza kuwa maneno ya Wakazi yamebeba nini na kama kilichoandikwa kimepokelewa vipi na ROMA, mwamba mwenye maua yake amejibu;

"Sikerwi hata kidogo na interviews zako, uko sawa kwenye mambo kadhaa✅✅ but hai-sound unyade kumuongelea mtu mara kwa mara kwenye interviews zako (hata kama wakikuuliza kuhusu mtu huyo) mind that….hata sisi huwa tunaulizwa sana tu na hao hao watangazaji kuhusu watu fulani, but tuna-opti ku-mute au kuskip hayo maswali!  Muda wa kuongelea watu ugeuze ongelea Art yako, push product zako, jiuze, jitangaze, jinadi wewe mwenyewe! Yani badilisha content ya interview yao, simama wewe ndo uwe content/wape content kuhusu wewe!  Unapewa 1hr la kufanya interview, promote album yako watu wajue ngoma zako, ww unamaliza lisaa zima kufanya hotuba/risala! Mziki wako hawataujua watu!!  CHANGE"

Katika mazungumzo yao, utagundua ROMA hataki azungumzwe katika mahojiano anayofanya WAKAZI kwenye TOUR yake na kumshauri atumie nafasi hiyo kujitangaza mwenyewe na vitu kama hivyo.

NINI MAONI YAKO KAMA MFUATILIAJI NA MFUASI WA MUZIKI NCHINI TANZANIA?

Post a Comment

Previous Post Next Post