Mganga wa Tiba Asili ajulikanaye kwa jina
la Ngusa Jilumba (58) pamoja na Mkewe Bugumba Mahola (54)
wameuawa papo hapo kwa kukwatwa na mapanga
pamoja na shoka baada ya kuvamiwa nyumbani kwao na watu
wasiojulikana katika Kijiji cha Sungamile Halmashauri ya Msalala
Wilayani Kahama Mkoani Shinyanga.
Na. Mwandishi Wetu, Sungamile Kahama Shinyanga.
Akizungumza eneo
la tukio katika Kijiji hicho, Mwenyekiti wa Kijiji Cha Sungamile
Charles Tungu amesema amezipata taarifa za mauaji hayo majira ya Saa nane Usiku
Januari 20, 2023 ambapo Jeshi la Ulinzi Shirikishi(Sungusungu) walishirikiana.
“Baada ya kupokea
taarifa za mauaji haya kwa kushirikiana na Jeshi la Ulinzi
Shirikikishi(Sungusungu) na Jeshi la Polisi kupiga mwano walikuja na mapanga na
walipitia shoka linalotumika kupasulia kuni wakalitelekeza shambani”amesema.
Aidha, ametoa wito kwa
Wananchi wa Kijiji chake kuacha kujichukulia sheria mkononi huku akiomba
Watalaam wa Kisaikolojia kuweza kuwasaidia msaada wa Kisaikolojia Watoto
walioachwa na marehemu ikiwemo mlemavu wa macho aliyekatisha ndoto zake za
kuendelea na elimu Chuo cha Serikali za Mtaa Hombolo kwani mara tu kumaliza
kidato cha nne alipofuka.
Ester Juma
ni binti manusura aliyeshuhudia Baba mkubwa na Mama
mkubwa wakiuwa ndani ya nyumba hiyo ambapo amesema yeye alikuwa
amelala chumba kingine ambapo alisikia mlango ukipigwa na kitu kizito kasha
kufunguliwa.
“Nilisikia mlango paa
, mama mkubwa na Baba mkubwa wakapiga kelele, mara nikasikia baba
analia na kudondoka chini ,mama alijificha akajitokeza akasema tuna laki saba
tunaomba tuwape , sauti ikasikika hiyo laki saba tunaweza kununua ng’ombe
sisi ??mama nikasikia tu mguu unakanyagwa paa akaacha na
kuongea sasa wakatoka , chumbani kwangu walinikuta baba mmoja
hivi na panga akanisonta walikuja saa saba nikasikia
nyumba ya pili kaka asiyeona anapiga kelele na
iliyotumika ni shoka ya hapa waliitelekeza shambani sasa tunaogopa sijui
tunaishije?amesema.
Watoto wa marehemu
akiwemo Lukala Ngusa Jilumba wamesikitishwa kutokea kwa tukioa hilo huku
wakiomba vyombo vya dola kuendelea kuchunguza zaidi ili kuwabaini waliofanya
unyama huo.
“Nasikitika sana kwa
wazazi wangu wawili kwa kufariki kwa siku moja kwa ajali mbaya ya namna hii ya
kukatwakatwa na mapanga, mimi hapa nina changamoto ya kutoona na sioni naomba
serikali ilifuatilie hili tukio maana mimi ni mlemavu wa macho tangu mwaka 2018
na wazazi wangu ndio nilikuwa nawategemea kwa kila kitu kama kuna uwezekano
mimi nikasaidiwe nipate matibabu na tutaishije kwa unyama uliofanyika ni ngumu
kuvumilia kwa sisi watoto”amesema.
Mzee Seni Jilumba ni
kaka wa marehemu amesema hajawahi kusikia mgogoro wowote kwa marehemu huku
jirani wa mji huo Masumbuko Doto amesema muda wa saa 7:45 usiku alitumiwa
ujumbe wa maandishi kwenye simu ndipo walichukua hatua za kuchukua filimbi na
kupiga mayowe ya sungusungu.
“Nilipokea ujumbe kuwa
tumevamiwa na tukachukua hatua za haraka kupiga mayowe na tulipoanza ukaguzi
tukakuta asubuhi shambani kuna bufa pamoja na shoka zimetupwa shambani ni tukio
la kusikitisha tunaiomba serikali itujengee na kituo cha polisi hapa
Sungamile”amesema.
Mtemi wa Jeshi la
Ulinzi Shirikishi(Sungusungu) Halmashauri ya Msalala Wilayani Kahama Mkoani Shinyanga
Bundu Mswaki Kahanya ameiomba Serikali kuongeza nguvu katika
kulisaidia jeshi hilo ili kuimarisha ulinzi zaidi .
“Sisi huwa
tunashirikiana sana na Serikali ila tunaiomba iongeze nguvu hasa vyombo vya
dola kushirikiana na sisi mfano kupata vifaa vinavyoweza kunasa mapema watu
wanaofanya vitendo kama hivi tuungane nguvu maana wakati mwingine
wahalifu wanakuwa na silaha nzito sisi hatuna namna”amesema.
Onesmo Daud ni Mtaalam
wa Sheria anasema watu waliopoteza maisha wamekoseshwa haki zao za
msingi za kuishi .
“Mtu anayefanya mauaji
anatakiwa apewe adhabu zake hivyo nasikitishwa na tukio hili naomba serikali
iongeze nguvu ya kutosha, elimu ya haki za binadamu ili jamii ipate kuwa na
uelewa kuhusu masuala mbalimbali ya haki ili kupunguza makosa jinai”amesema.
Marehemu wote
wawili Mke na Mme wamezikwa nyumbani kwao katika Kijiji cha
Sungamile Wilayani Kahama Mkoani Shinyanga na waliuawa kwa
kujeruhiwa kichwani na shingoni na kufa papo hapo kutokana na kuvuja damu
nyingi huku mganga wa Tiba Asili Ngusa Jilumba akizikwa kwa kimila akiwa
amekalishwa kwenye kaburi na tayari watu watatu wanashikiliwa na Jeshi la
Polisi kwa upelelezi zaidi dhidi ya tukio hilo.
Post a Comment