Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe.Dkt. Doto Biteko, leoamekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa China nchini Tanzania, Chen Mingjian ambapo walizungumza masuala mbalimbali ikiwemouhusiano uliopo kati ya Tanzania na China na uwekezaji kwenye miradiya Nishati.

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt. Doto Biteko (katikati)
akizungumza na Balozi wa China nchini Tanzania, Mhe. Chen Mingjian na
Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Mhandisi Felchesmi Mramba jijini Dar
es Salaam tarehe 24 Novemba 2023.


Mazungumzo hayo yamefanyika jijini Dar es Salaam tarehe 24 Novemba2023 na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali kutoka Wizara ya Nishati naUbalozi wa China nchini Tanzania wakiongozwa na Katibu Mkuu wa Wizaraya Nishati, Mhandisi Felchesmi Mramba.Dkt.Biteko, amemweleza Balozi Mingjian kuwa Tanzania inathaminiuhusiano mzuri ulipo kati ya nchi hizi mbili ambao mwakani utafikiamiaka 60 huku akitaja miradi mbalimbali kwenye Sekta ya Nishati naMadini ambapo kuna Wawekezaji/Wakandarasi kutoka China.“ Sisi Tanzania tunaufurahia na kuuthamini uhusiano mzuri uliopo nahapa kuna kampuni nyingi kutoka China zinazofanya kazi kwenyeuchimbaji madini ikiwemo madini ya viwandani na uchenjuaji madini, piakwenye miradi ya Nishati kuna kampuni za Kichina zinafanya kazi mfanokampuni ya TBEA inayojenga laini ya umeme ya kV 400 kutoka Chalinzehadi Dodoma, na mradi wa kusafirisha umeme wa kV 400 kutoka Tanzaniakwenda Zambia.” Amesema Dkt. BitekoKuhusu miradi hiyo ya usafirishaji umeme kutoka Chalinze hadi Dodomana mradi wa TAZA, Dkt. Biteko ametoa wito kwa Serikali ya Chinakuiwezesha kwa namna mbalimbali kampuni hiyo ikiwemo kifedha iliitekeleze miradi hiyo kwa ufanisi na kwa wakati kutokana na umuhimu wamiradi hiyo.Katika hatua nyingine, Dkt. Biteko amesema kuwa, nchi ya Tanzania badoina uhitaji wa umeme wa kutosha utakaotokana na vyanzo mbalimbaliikiwemo maji hivyo amekaribisha kampuni kutoka China kuja kuwekezakwenye eneo hilo.Dkt. Biteko amemweleza pia Balozi, Mingjian kuhusu mradi wa Bomba laMafuta Ghafi la Afrika Mashariki (EACOP) ambapo ameeleza kuwa nchi yaUganda na Tanzania zinauthamini mradi huo na zinaendelea nautekelezaji wake ambapo kampuni kutoka China ya CNOOC ni moja ya Wabiawa mradi huo.Kwa upande wake, Balozi wa China nchini, Mhe. Chen Mingjian nayeameeleza jinsi China inavyouthamini ushirikiano uliopo kati yaTanzania na China na kielelezo kikiwa ni ujio wa Rais wa nchi hiyonchini Tanzania mwaka 2013 na mahusiano mazuri yaliyopo kati ya Raiswa Tanzania, Dkt, Samia Suluhu Hassan na Rais wa China, Xi Jinping.Kuhusu suala la kampuni za China kuja kuwekeza Tanzania kwenye miradiya Nishati amesema kuwa, atazikaribisha kampuni hizo, huku akitoleamfano kampuni ya Synohydro ambayo inafanya vizuri ujenzi wa miradi yauzalishaji umeme wa maji.

Post a Comment

Previous Post Next Post