Mganga Mkuu wa Serikali Prof.Tumaini Nagu akiteta jambo na
Mkurugenzi wa Huduma za Tiba Wizara ya Afya Prof. Pascal Ruggajo katika
kikao
baina ya Wizara ya Afya na wadau cha kutoa maoni kuhusu Mpango Jumuishi na
Endelevu wa kuratibu Wahudumu wa Afya Ngazj ya Jamii (Stakeholders Meeting on
Integrated and Coordinated Community Healthy Workers Program).
Na Mwandishi Wetu.
Akizungumza katika kikao hicho kilichofanyika Jijini Dar Es Salaam Mganga Mkuu
wa Serikali Prof. Nagu amesema Wahudumu wa Afya Ngazi ya Jamii wana umuhimu
mkubwa katika utoaji wa huduma za afya ngazi ya jamii hivyo kupitia kikao hicho
cha kupitia Mpango huo itakuwa na chachu kubwa katika uimarishaji wa huduma za
afya ngazi ya jamii.
“Wahudumu wa Afya Ngazi ya Jamii wana umuhimu kwani wao ndio wanaosaidia kutoa
elimu ya afya ngazi ya chini kabisa ya kijiji hivyo kupitia Mpango Jumuishi
itakuwa chachu kubwa katika utoaji wa huduma za afya ngazi ya jamii mfano elimu
juu ya lishe, utapiamlo” amesema.
Mkurugenzi wa Idara ya Kinga kutoka Wizara ya Afya Dkt. Ntuli akizungumza katika kikao
baina ya Wizara ya Afya na wadau cha kutoa maoni kuhusu Mpango Jumuishi na
Endelevu wa kuratibu Wahudumu wa Afya Ngazj ya Jamii (Stakeholders Meeting on
Integrated and Coordinated Community Healthy Workers Program).
Naye Mkurugenzi wa Idara ya Kinga kutoka Wizara ya Afya Dkt. Ntuli Kapologwe
amesema Wahudumu wa Afya Ngazi ya Jamii wana mchango mkubwa katika kusambaza
ujumbe kuhusu masuala mbalimbali ya afya hasa katika eneo la kinga dhidi ya
magonjwa ngazi ya jamii, huku Mkurugenzi wa Huduma za Tiba Prof. Pascal Ruggajo
akisema kupitia Programu hiyo inasaidia katika kuhakikisha suala la tiba halina
kikwazo.
Kwa upande wake Mkurugenzi Msaidizi Sehemu ya Elimu ya Afya kwa Umma kutoka
Wizara ya Afya Dkt.Tumaini Haonga ameainisha baadhi ya mikakati kabambe
inayotumika katika uimarishaji wa huduma za afya ngazi ya jamii kuwa ni pamoja
na kutoa elimu ya afya katika mapambano ya magonjwa mbalimbali ikiwemo Virusi
vya UKIMWI na UKIMWI, Malaria, Kifua Kikuu (TB), magonjwa ya mlipuko kama
Kuhara ikiwemo Kipindupindu.
Ikumbukwe kuwa kuanzishwa kwa Mpango Jumuishi na Endelevu wa Kuwatumia Wahudumu
wa Afya Ngazi ya Jamii una lengo la kuharakisha upatikanaji wa huduma bora za
afya kwa wote hususan katika ngazi ya msingi ambapo inalenga kuvifikia vijiji
12,318, mitaa 4,263 na vitongoji 64,384 nchi nzima.
Post a Comment