YOUR FUTURE IS CREATED BY WHAT YOU DO TODAY, NEVER TOMORROW

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Prof. Joyce Ndalichako amekutana na kufanya mazungumzo na Menejimenti ya Ofisi hiyo tarehe 7 Juni, 2023 katika jengo la OSHA, jijini Dodoma.


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Prof. Joyce Ndalichako akiongoza kikao cha majadiliano alipokutana na menejimenti ya ofisi yake katika jengo la OSHA leo tarehe 7 Juni, 2023 jijini Dodoma.
Kaimu Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Bw. Leonard Mchau (aliyesimama) akieleza jambo wakati wa kikao hicho.


Na Mwandishi wetu.


Lengo la kikao hicho ni kufanya majadiliano kuhusu maendeleo ya ukarabati na marekebisho ya Vyuo vinne (4) vya Ufundi Stadi kwa Watu wenye Ulemavu, hatua iliyofikiwa ujenzi wa Vyuo vitatu (3) vya Watu wenye Ulemavu, Mpango wa Taifa wa Watu wenye Ualbino na Madeni ya Waajiri ambao hawajawasilisha michango kwenye Mifuko ya Hifadhi ya Jamii.

 

Sehemu ya wajumbe wa menejimenti wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Prof. Joyce Ndalichako (hayupo pichani) wakati wa kikao hicho.

Prof. Ndalichako pia amewataka viongozi hao kuendelea kuchapa kazi kwa weledi na ufanisi katika kutekeleza majukumu yao ili kufikia azma ya Serikali na wananchi wanaowahudumia.

 

Vile vile, Mhe. Ndalichako amesisitiza menejimenti hiyo kuendelea kutangaza mafanikio na mambo makubwa yanayofanywa na serikali kwa maslahi ya taifa.


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Prof. Joyce Ndalichako (kulia) na Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Patrobas Katambi wakipitia kitabu cha Mpango wa Taifa kwa Watu wenye Ualbino 2023/2024 – 2027/2028.


Post a Comment

Previous Post Next Post