YOUR FUTURE IS CREATED BY WHAT YOU DO TODAY, NEVER TOMORROW


Tangu siku ya jana mamia kwa maelfu ya mahujaji walikusanyika kwa ibada katika eneo la Mlima Arafa ikiwa ni kilele cha Hija ambayo ni moja ya nguzo kuu tano za dini ya Uislamu.  

Licha ya hali ya joto kali, waumini hao walisimama kwenye viwanja vya Arafa kuomba dua, eneo ambalo inaaminika Mtume Muhammad alitoa hotuba yake ya mwisho kwa umma wa Waislamu.   

"Nina furaha sana kufanya ibada ya Hijja. Ninamshukuru Mwenyezi Mungu. Hatutamani kuondoka eneo hili la (Mlima Arafa). Tizama umma wote huu unashiriki Hijja, tunajihisi tumetakasika." Alisema Samaher al Faisal, hujaji kutoka nchini Syria.  

HHii Leo, mahujaji watashiriki zoezi la ishara la kumpiga mawe shetani wakati waumini wengine ulimwenguni wakishehereka sikukuu ya Eid inayojumisha uchinjaji wa wanyama.

Post a Comment

Previous Post Next Post