Wawakilishi kutoka Mashirika mbalimbali yasiyo kuwa ya Kiserikali hapa nchini (NGO’s) yanayotekeleza miradi ya afya wamesema Elimu ya Afya kwa Umma, Idara ya Kinga, Wizara ya Afya ni Mama na Baba katika kufanikisha utekelezaji wa Miradi yao hapa nchini.



Na. Elimu ya Afya kwa Umma.

Wakizungumza katika kikao kazi cha pamoja kati ya wadau wa Maendeleo na Serikali kuhusu kuainisha vipaumbele na mikakati ya utekelezaji (Health Promotion priority interventional activities) kwa mwaka 2023/2024 kinacholenga kuwa na Mpango wa Utekelezaji wa Afua za Elimu ya Afya kwa Umma (Health Promotion Annual Work Plan) na kuainisha vyanzo vya fedha za utekelezaji wa afua za kipaumbele baadhi ya wadau hao akiwemo mwakilishi Shirika la Afya Duniani(WHO) Jeryy Mlembwa  wamesema kuwa Wizara ya Afya kupitia Elimu ya Afya kwa Umma  ni muhimu kuweka nguvu ya pamoja katika ushirikiano.

Baadhi ya Washiriki wa  kikao kazi cha pamoja kati ya Wadau wa Maendeleo na Serikali kuhusu kuainisha vipaumbele na mikakati ya utekelezaji (Health Promotion Priority interventional activities) kwa  mwaka 2023/2024  kinachoendelea jijini Arusha ikiwa leo ni siku ya nne

“Wizara ya Afya kupitia Sehemu ya Elimu ya Afya kwa Umma mmepewa Majukumu kama walezi wetu katika utekelezaji wa miradi yetu ya Afua za Afya hivyo niwaombe na wadau wenzangu  kuanzia leo tutambue tunapokwenda kutekeza miradi ya  Elimu ya  Afua za Afya tusiende moja kwa moja huko bila kuwashirikisha Elimu ya Afya kwa Umma hasa Masuala ya Uelimishaji ,sisi kama WHO mojawapo ya kanuni tunazosisitiza  wadau ni kuwa na mfumo  unaotuunganisha pamoja katika utekelzaji wa afua za afya” amesema   Mlembwa Mwakilishi WHO.

"Elimu ya Afya kwa Umma ni kama Moyo wa Wizara ya Afya, sisi sote kama wadau tunapotekeleza masuala mbalimbali ya Afya ni muhimu kuwashirikisha na tukifanya bila uwashirikisha ni sawa na bure "amesema Dkt. May Bukuku mwakilishi kutoka UNICEF.

Baadhi ya Washiriki wa  kikao kazi cha pamoja kati ya Wadau wa Maendeleo na Serikali kuhusu kuainisha vipaumbele na mikakati ya utekelezaji (Health Promotion priority interventional activities) kwa  mwaka 2023/2024  kinachoendelea jijini Arusha ikiwa leo ni siku ya nne

"Tunapotekeleza miradi ya afua za Afya huko kijijini  hasa  afya ngazi ya jamii lazima Wizara ya Afya kupitia Elimu ya Afya kwa Umma ijue na inapojua yenyewe inakuwa na mchango mkubwa katika masuala ya Uelimishaji hivyo ni Muhimu kuhishirikisha Elimu ya Afya kwa Umma"amesema Mussa Lunnyonga Mwakilishi AMERICARES.

Beatrice Mkani kutoka SIKIKA amesema Wizara ya Afya ni mlezi Mkuu katika utekelezaji wa Majukumu yao.

"Elimu ya Afya  kwa Umma, Wizara ya Afya  ndio Mlezi mkubwa anayetekeleza masuala ya Promotion kwa  afua za Afya hivyo tunapokwenda kutekeleza tusiwaache nyuma tupite kwanza kwao kwa ushauri na ushirikiano kwa hakika tunaweza kuifikia jamii katika  mwelekeo wenye Mpangilio zaidi" amesema Beatrice.  

Kwa upande wake Mwenyekiti wa kikao hicho ambaye ni mwakilishi kutoka  Elimu ya Afya kwa Umma, Idara ya Kinga, Wizara ya Afya, John Yuda amesema wao kama Serikali wanatambua mchango Mkubwa unaotolewa na Mashirika yasiyokuwa ya Kiserikali hivyo jitihada za pamoja zinahitajika hasa katika suala la uelimishaji.

Mwakilishi Kutoka Elimu ya Afya kwa Umma, Idara ya Kinga,Wizara ya Afya,John Yuda akizungumza katika kikao cha kuandaa Mpango Kazi elimu ya afya kwa umma 2023/2024 kwa kushirikiana na wadau mbalimbali

“Tunatambua mchango Mkubwa unaotolewa na Mashirika Yasiyo ya Kiserikali kinachohitajika tu ni wote tushirikiane hasa katika afua hii ya Elimu ya Afya ”amesema Yuda.

Naye  Msimamizi wa  Ubunifu na Maudhui, Sehemu ya Elimu ya Afya kwa Umma, Wizara ya Afya James Mhilu amesema mitandao ya kijamii katika ulimwengu wa sasa ina nguvu na kasi kubwa  ndio maana Elimu ya Afya kwa Umma imewekeza zaidi huko na kuwaondoa hofu wadau kuwa wanapowekeza huko ujumbe unafika kwa jamii kwa wakati na haraka zaidi.

Msimamizi wa  Ubunifu na Maudhui, Elimu ya Afya kwa Umma,Wizara ya Afya James Mhilu akichangia katika kikao cha kuandaa Mpango Kazi elimu ya afya kwa umma 2023/2024 kwa kushirikiana na wadau mbalimbali kinachoendelea jijini Arusha.

“Katika Ulimwengu wa sasa Mitandao ya Kijamii ina nguvu sana na unaweza kujiuliza kitu kimesambaa mtandaoni lakini unashangaa habari ya kitu hicho imefikaje kijijini sehemu ambako hakuna Internet? kuna mbinu mbalimbali zinazotumika mfano  mtu mwenye simu yenye uwezo wa Mtandao (Internet) anaichukua kisha anasambaza kwa ujumbe wa kawaida” amesema James.

Hivyo ,kutokana na mitandao ya kijamii kuwa nguvu zaidi ,hivi karibuni  jijini Dodoma Waziri wa Habari ,Mawasiliano na Teklonojia ya Habari, Nape Nnauye alizindua Taasisi ya Waandishi wa Habari   wa Mtandaoni (TOMA] yenye Makao Makuu yake jijini Arusha.

Mratibu wa Elimu na Mabadiliko ya Tabia Elimu ya Afya kwa Umma, Idara ya Kinga, Wizara ya Afya Peter Mabwe amesema kikao hicho kitaleta mabadiliko makubwa katika utekelezaji wa majukumu hasa katika afua za Afya.

Mratibu wa  Elimu na Mabadiliko ya Tabia Elimu ya Afya kwa Umma, Idara ya Kinga, Wizara ya Afya Peter Mabwe akichangia katika kikao cha kuandaa Mpango Kazi elimu ya afya kwa umma 2023/2024 kwa kushirikiana na wadau mbalimbali.

Ikumbukwe kuwa  kikao kazi cha pamoja kati ya Wadau wa Maendeleo na Serikali kuhusu kuainisha vipaumbele na mikakati ya utekelezaji (Health Promotion priority interventional activities) kwa mwaka 2023/2024   kilianza tarehe 13 Februari, 2023 na kitaendelea hadi tarehe  17, Februari, 2023 huku kikihusisha  washiriki  kutoka Wizara ya Afya, OR-TAMISEMI,  Wadau mbalimbali   ikiwemo mwakilishi kutoka Shirika la Kuhudumia  Watoto Duniani (UNICEF, PSI, USAID,PACT, TCDC, SIKIKA, D-Tree, Marie Stopes, World Vision, Save the Children, TRCS,EGPAF, AMERICARES, Mkapa Foundation, Girl Effect Apotheker, na T-Marc Tanzania.

Hata hivyo kikao kazi hicho ,kitaleta mabadiliko katika utekelezaji wa afua mbalimbali za afya  hapa nchini ambapo leo ni siku ya tano   tangu kianze siku ya Jumatatu huku wadau wengine wakishiriki kwa njia ya Mtandao.

 

Post a Comment

Previous Post Next Post