YOUR FUTURE IS CREATED BY WHAT YOU DO TODAY, NEVER TOMORROW


ILALA ZONE COLLEGE BASH ni Mashindano ya kumpata Mfalme wa Bongo Flavour kutoka katika vyuo mbalimbali vinavyopatikana katika Wilaya ya ILALA. 

Je, unajihisi umetengwa? LA HASHA! Tamasha hili litahusisha wasanii mbalimbali wenye vipaji kutoka mitaa mbalimbali ya jiji la DAR ES SALAAM na vitongoji vyake, kushiriki na kushinda.

Haina #kashikashi, Mshindi atajinyakulia pesa Taslimu juu ya STAGE ya peke yake. Pia atajiapatia fursa ya kurekodi audio track ama wimbo mmoja na kufanyiwa video huku vigezo na masharti vikizingatiwa.

Kama hiyo haitoshi, Mshindi wa #ILALA_ZONE_COLLEGE_BASH, atapata nafasi ya kufanyiwa #PROMOTION ya kazi zake na kutengenezewa #CONNECTIONS mbalimbali zitakazomuwezesha kutimiza malengo yake kimziki.
Tamasha hili litafanyika ndani ya ukumbi wa #TUPENDANE_BAR unaopatikana maeneo ya #BUGURUNI_ROZANA, Haina kupotea.

Msanii atakayeshiriki atatakiwa kulipia form ya ushiriki inayopatikana kwa shilingi 10,000/= tu ya kitanzania. Wasanii mbalimbali ambao tayari wanafanya vizuri kupitia mziki wa BONGO FLAVOR watashiriki nasi kutupatia burudani na SUPRIZE kama zote. Akiwemo #BENSON bwana #HAUZIMI, #BABY_MADAHA na wengine wengi.

KWA MAELEZO ZAIDI ACHA COMMENT YAKO UPATIWE NAMBA YA SIMU.


Post a Comment

Previous Post Next Post