YOUR FUTURE IS CREATED BY WHAT YOU DO TODAY, NEVER TOMORROW
Dkt. John Pombe Magufuli amemteua George Boniface
Simbachawene kuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na
Mazingira.
Simbachawene anachukua nafasi ya Mhe. January Yusuf Makamba ambaye uteuzi
wake umetenguliwa.
Wakati huo huo, Mhe. Rais Magufuli amemteua Hussein Mohamed Bashe kuwa
Naibu Waziri wa Kilimo.
Bashe anachukua nafasi ya Mhe. Innocent Lugha Bashungwa ambaye aliteuliwa
kuwa Waziri wa Viwanda na Biashara.
Katika hatua nyingine, Mhe. Rais Magufuli amemteua Balozi Dkt. Martin
Lumbanga kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Udhibiti wa
Ununuzi wa Umma (PPRA).
Balozi Dkt. Lumbanga ameteuliwa kushika nafasi hiyo kwa kipindi cha pili.
Uteuzi wa viongozi hao ulianza kufanya kazi siku ya jana tarehe 21 Julai,
2019.
TIZAMA VIDEO HAPA CHINI:
Post a Comment