YOUR FUTURE IS CREATED BY WHAT YOU DO TODAY, NEVER TOMORROW

Naibu
waziri wa maji Juma Aweso ametoa wiki tatu kwa kampuni ya mavonoa’s
kuhakikisha wanakamilisha ujenzi wa mradi wa maji wa Sawala uliopo jimbo
la Mufindi kusini katika wilaya ya Mufindi mkoani Iringa

NAIBU
waziri wa maji Juma Aweso akimbana mkandarasi wa kampuni ya mavonoa’s
kwa kushindwa kukamilisha ujenzi wa mradi wa maji wa Sawala uliopo jimbo
la Mufindi kusini katika wilaya ya Mufindi mkoani Iringa
NA FREDY MGUNDA,IRINGA.
NAIBU
waziri wa maji Juma Aweso ametoa wiki tatu kwa kampuni ya mavonoa’s
kuhakikisha wanakamilisha ujenzi wa mradi wa maji wa Sawala uliopo jimbo
la Mufindi kusini katika wilaya ya Mufindi mkoani Iringa.
Akizungumza
mbele ya wananchi,wabunge na wafanyakazi wa halmashuri hiyo,waziri
Aweso alisema kuwa amekuwa akipokea malalamiko mengi ya mkandasi huyo
ambaye amekuwa hana mahusiano mazuri na viongozi wa halmashauri hiyo.
“Mimi
niseme ukweli nakupa wiki tatu kuhakikisha unamalizia ujenzi wa mradi
wa maji wa Sawala la sivyo utaniona mbaya na mimi ni mkali kweli kwa
wakandasi wamepewa kazi na serikali na wanashindwa kutekeleza mradi kama
ambavyo mkabata ulisema hivyo nakupa wiki tatu kuhakikisha wananchi
wanapata maji” alisema Aweso
Aweso
alisema serikalia ya awamu ya tano haita kubari kumuanda mkandarasi
yeyote Yule aliyepewa kazi na serikali anashindwa kukamilisha mradi
wakati fedha amepewa,mkandarasi huyo atachukuliwa hatua za kisheria
haraka sana kwa kuwa saizi hakuna mtu kutumia vibaya pesa za serikali
kama ilivyokuwa huko nyuma.
“Walizoea
kuzichezea pesa za serikali miaka ya huko nyuma kwa sasa hakuna
mkandarasi tayeweza kuichezea serikali ya awamu hii kwa kuwa sisi
wateule wa Rais wetu Dr John Pombe Magufuli hakuna anayekubari
kutumbuliwa kisa wakandarasi kufanya vibaya kwenye miradi waliyopewa”
alisema Aweso
Aidha
naibu waziri Aweso aliwatoa hofu viongozi wa halmashuri ya wilaya ya
Mufindi kuhusu mkandarasi huyo kuwa akishindwa kutekeleza mradi huo
ndani ya wiki tatu hizo basi sheria itachukua mkoando wake.
“Mkuu
wa wilaya,mbunge,mkurugenzi na mwenyekiti wa halmashauri
niwahakikishieni kuwa nitatakuja tena tarehe mbili mwezi wa tatu hapa
kuja kuangalia kuwa huu mradi umefikiwa wapi na makubariano yetu
ameyatekeleza mkandarasi huyu” alisema Aweso
Awali
mkuu wa wilaya ya Mufundi Jamhuri William alimueleza naibu waziri kuwa
mkandarasi huyoamekuwa anaidharau serikali kwa kuwa mara kwa mara
ameandikiwa barua na serikali ya wilaya lakini hajawahi kujibu hata mara
moja kitendo kinachoashiria dharau.
“Huyo
mkandarasi amekuwa anatusumbua sana maana tunamuita mara kwa mara
hataki kuitika wito wetu hivyo hizo ndio dharau kubwa kiasi kwamba
anashindwa hata kuendelea kutekeleza mradi huu ambao wananchi
wanategemea kuwa mkombozi wao” alisema Jamhuri William
Mkuu
wa wilaya alisema kuwa atamkamata na kuwa ndani mkandarasi huyo kwa
kuwa anachelewesha kuteleza mradi huo wa maji na kusababisha wananchi
kuichukia serikali kwa kusema kuwa wametoa ahdi hewa kitua ambacho sio
kweli.
“Mheshimiwa
naibu waziri hapa Sawala tunashindwa hata kufanya mikutano ya hadhara
kwa ajili ya huu mradi wa maji ambao mwazoni wananchi walijenga imani
kubwa wakati wa kusainiana mkataba wa kutekeleza mradi huu” alisema
Jamhuri William
Akitoa
malalamiko hayo mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Mufindi Festo
Mgina alimwambia naibu waziri wa maji Juma Aweso kuwa hamhitaji tena
huyo mkandarasi kwa kuwa amekuwa kikwazo cha kuleta maendeleo ya
wananchi kwa kushindwa kutekeleza mradi huo wa maji.
“Huyu
kwetu ni kero kubwa mno mheshimiwa naibu waziri wa maji,sisi kama
halmashauri hatupo tayari kufanya kazitena na huyu mkandari kwa ujeuri
wake na kushindwa kuiheshimu sekali ya wilaya kwa kushindwa kumtua ndo
mwanamke” alisema
Nao
baadhi ya wananchi walijitokeza hapo walimwambia naibu waziri kuwa
mkandarasi huyo hafanyi kazi ipasavyo kwa kuwa amesikia waziri unakuja
ndio na yeye ameanza kazi jana tu ya kukarabati tenki hili la maji ili
ukifika uone kama yupo anafanya kazi wakati sio kweli.
Hata
hivyo naibu waziri Juma Aweso alimalizia kwa kusema kuwa ifikapo tarehe
mbili mwezi wa tatu mradi huo uwe umekamilika na wananchi waweze kupata
maji na kufanikisha adhima ya Rais ya kumtua ndoo mwanamke.
Post a Comment